Na Hamisi Magendela
MWENYEKITI wa klabu ya Simba inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Ismail Aden Rage, amesema yuko katika mchakato wa kuhakikisha timu ya taifa (Taifa Stars) inafanya vizuri katika mchezo dhidi ya Chad.
Akizungumza Dar es Salaam juzi Rage, alisema haoni sababu ya kushindwa katika mchezo huo unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.
"Nilisikitishwa sana kukosa nafasi katika mashindano yaliyopita ya kutafuta tiketi ya kwenda michuano ya Afrika, lakini katika mchezo dhidi ya Chad naamini mikakati ninayoipanga itasaidia timu ya taifa kushinda na kwenda katika hatua inayofuata," alisema Rage.
Alisema kupoteza mchezo dhidi ya Chad itasababisha Stars kukaa bila ya mashindano kwa miaka miwili, hivyo kutokana na hilo jitihada zifanyike kuhakikisha Stars inashinda mchezo huo.
Pia, aliwaomba mashabiki kuonesha uzalendo pindi timu ya taifa inapocheza ili kuiongezea hali ya kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa.
"Mashabiki wengi inapocheza Taifa stars hawashtuki kama zinapocheza timu za watani wa jadi katika mchezo wa mpira wa miguu Simba na Yanga, hivyo umefika wakati wa kuonesha uzalendo kwa timu ya taifa," aliongeza Rage.
Wednesday, October 19, 2011
New
Rage asapoti mikakati ya Stars
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment