Twanga wawaonjesha wadau Dunia Daraja - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 19, 2011

Twanga wawaonjesha wadau Dunia Daraja

Na Asha Kigundula
ONESHO maalum kwa wadau wa muziki wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta’ la utambulisho wa albamu mpya Dunia Daraja lililofanyika jana kwenye Ukumbi wa Maisha Club limefana.
Katika onesho hilo, wadau mbalimbali wa muziki walihudhuria na kupewa nafasi ya kula keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya usiku huo.
Twanga ilianza kupiga nyimbo nne za albamu zilizopita na baadae kutambulisha nyimbo zake moja moja kuanzia ule uliobeba albamu, Dunia Daraja na nyinginezo za albamu za nyuma.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka aliwashukuru mashabiki kwa kufika katika onesho hilo na kuwaomba wafike kwa wingi siku ya uzinduzi rasmi hapo Novemba 6 kwenye Viwanja vya Leaders Club.
Naye Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Poulsen na washinda wa mwa mwaka huu wa Bongo Star Search (BSS Socond Chance) nao walihudhuria onesho hilo kama sehemu ya kutambua mchango wa bendi hiyo kwa mwanamuziki, Haji Ramadhani aliyeibuka na kitita cha sh milioni 40 cha mashindano ya mwaka huu.
Rita alimshukuru Baraka kwa malezi mema ya Haji mpaka kutwaa taji hilo na kuwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi za mwanamama huyo ambaye alimuomba Haji kujiunga katika bendi yake baada ya mashindano ya mwaka jana.

No comments:

Post a Comment