- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 23, 2012

Na Asmah Mokiwa
WADAU wa soka nchini wamelaani vikali vitendo vya waamuzi kuhusishwa na kuchukua rushwa kwa ajili ya kuzipendelea timu pinzani.
Akizungumza na Magendela Blogspot Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo cha vipaji cha Talent Academy, Ali Akida, alisema ameshangazwa na waamuzi wanaochezesha ligi za mchangani pia kushukiwa katika madai ya kuchukua rushwa.
Alisema timu yake ilishiriki kombe la jezi na mbuzi, ambalo lilikuwa likifanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, lakini waamuzi wa mechi walizocheza walikuwa wakituhumiwa kuchukua rushwa hadi ya sh. 5,000 na kuchezesha mechi vile walivyoambiwa.
"Ni tamaa za fedha na kutojua vyema sheria za uamuzi wa soka, kwani mtu anadiriki kuchukua hata sh. 5,000 ili awakwamishe msishinde katika mechi zenu, si kitu cha kufurahisha," alisema Akida.
Alisema hali kama hiyo ikiendelea itaweka sura mbaya ya mchezo wa soka nchini, kwani soka litatawaliwa na rushwa kwa waamuzi na si wachezaji kujituma uwanjani.
"Itafikia wakati hali hii itafika hadi kwenye Ligi Kuu kama kwenye ligi za mchangani hali iko hivi, na viongozi watakuwa hawafanyi usajili mzuri kwa kuwa wanajua wao watatoa fedha na watashinda mechi zao," alisema Akida.

No comments:

Post a Comment