Shabiki Arusha atwaa pikipiki ya Simba
Mwandishi wetu
SHABIKI wa timu ya soka ya Simba mkoani Arusha, Abubakar Hamisi, ameibuka kidedea katika droo ya bahati nasibu katika kampeni ya 'changia Simba' inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya Push Mobile Media na klabu hiyo.
Katika bahati nasibu hiyo, Hamisi, ambaye ni dereva taxi, amejinyakulia zawadi ya pikipiki yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 3.
"Droo kubwa itafanyika Julai na mshindi atajinyakulia bajaji," alisema Rashid na kuongeza kuwa mashabiki wanatakiwa kuandika neno Simba na kutuma kwenda 15678 kuingia katika bahati nasibu hii.
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema ushindi wa shabiki huyo ni uthibitisho tosha kwamba mashabiki wao wanashinda katika bahati nasibu hiyo.
"Naomba wanachama na mashabiki wetu wajitokeze kushiriki katika bahati nasibu hii kwani ni moja ya kuichangia klabu ya Simba iweze kujiendesha na kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya Tanzania," alisema Kamwaga.
Mshindi atazawadiwa zawadi yake ndani ya wiki mbili kuanzia sasa, na kampuni ya Push Mobile Media itagharimia gharama za usafiri na kulala wakati wa kuja hapa jijini.
Alisema kuwa kwa sasa wamebakiza piki piki moja na bajaj ambazo drow yao itachezeshwa siku moja.
Wednesday, May 23, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment