NA MAGENDELA HAMISI
MBUNGE wa chama Cha upinzani nchini Kenya cha ODM, Paul Owino 'Babu Owino' amewataka vijana hususan wa chama cha ACT Wazalendo kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi mbalimbali nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Ngome ya Vijana wa ACT, ambao umetumika kuwachagua viongozi wao watakaodumu madarakani kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
"Vijana amkeni, mjiipambanie ili mjinasue kwenye dimbwi la umasikini, mkikaa nyuma hakuna atakayewapambania katika chaguzi zijazo kuanzia Serikali za mitaa, udiwani na ubunge jitokezeni mgombee ili muwe chachu ya mabadiliko.
"Msiwe waoga kumbukeni, hayati Mwalimu Nyerere, Kwame Nkuruma na wengine walijitokeza kuwania nafasi za uongozi wakiwa vijana nanyi mnatakiwa kuwa hivyo, " amesema.
Ameongeza kuwa anajua vijana wengi wanatokea katika familia masikini hivyo wanatakiwa kujipambania na kuwasisitiza jukumu lao kubwa ni kuketa mabadiliko katika Taifa la Tanzania kwa kuzika na kupambana na rushwa pamoja na ufisadi
Owino ambaye ni Mbunge wa ODM katika akaunti ya Embakasi Mashariki, amesema maendeleo ya taifa hili yapo mikononi mwa vijana kwa kujenga chama na nchi kwa ujumla
Pia aliwasitiza kuwa siasa sio chuki wala uadui wanachotakiwa ni kushindana kwa hoja na si vinginevyo ili kuleta amani na utulivu nchini na siasa isiwe chanzo cha machafuko.
Naye Katibu Mkuu wa ACT, Ado Hashimu aliwataka vijana hao kujenga chama kwanza kuanzia ngazi ya msingi ili kufanikisha kupata ushindi mnono katika chaguzi zijazo.
"Tunashukuru ACT tunao vijana wenye moyo huo na hatuwezi kutimiza malengo bila ya kuwa na vijana wanaojitolea na kuwa tayari kwa mapambano bila woga kwani siasa si lelemama," amesema.
No comments:
Post a Comment