DKT. LWAITAMA AKERWA KUZODOANA KWA VIONGOZI VYAMA VYA UPINZANI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, March 1, 2024

DKT. LWAITAMA AKERWA KUZODOANA KWA VIONGOZI VYAMA VYA UPINZANI

 


NA MAGENDELA HAMISI

WAZEE wa Mabaraza ya Vyama Vya Siasa nchini wamehimizwa kujenga ushirikiano na vyama vingine huku akikerwa kuzodoana na kudharauliana kwa viongozi wa Vyama Vya Upinzani. 

  

 Wito huo umetolewa leo Machi Mosi, 2024 jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa  Bodi ya Wadhamini  wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt.Azavel Lwaitama katika Mkutano Mkuu wa Ngome ya Wazee ya  Chama Cha ACT Wazalendo. 


Amesema kuwa mwaka 2015 ndio kielelezo ama mfano sahihi kutokana na upinzani kufanya vizuri katika uchaguzi huo kutokana na kuunganisha nguvu ya pamoja na si vizuri  kuona baadhi ya vyama kujiona vya kipekee zaidi ya vingine na kuanza kuzodoana.


Dkt. Lwaitama ambaye ni mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amefafanua kuwa kushirikiana kutasaidia tena kwa vyama hivyo kufanya vizuri tena.


"Naamini kama kusingekuwa na figisu ni dhahiri wapinzani wangekuwa wameshika dola, hivyo hakuna namna nyingine ya wapinzani kufanikiwa kushinda uchaguzi kama  hakutakuwa na ushirikiano kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi Mkuu wa 2015,"amesema.


 

"Kuna wakati nawauliza CHADEMA kwa ninj mnadharau na kuzodoa vyama vingine, naomba wazee wa ACT kuhakikisha mnahimiza ushirikiano na vyama  vingine hali itakayosaidia kufanya vizuri katika uchaguzi ujao, " amesema.


Dkt. Lwaitama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, amewasisitiza Wazee wa ACT Wazalendo wasisite kuzungumza na viongozi wa vyama vingine wanapoona wanafanya vitu tofauti na dhamira iliyopo. 


Pia amewataka kuwa washauri wazuri kwa vijana na kupunguza jazba hususan inapotokea kwenye chama chao au kingine ili kuleta utulivu na amani nchini.


Naye Kamishna Msaidizi mstaafu wa Jeshi la Polisi, Jamal Rwambo amesema katika vyama kuna changamoto kubwa ya rushwa hususan katika chaguzi, hivyo ni vizuri Wazee wa ACT, wakawa nguzo ya kudhiti hilo jambo ambalo litakuwa limeasidia taifa kupambana  na rushwa.


Naye Sheikh, Issa Ponda amesema kuwa kama kiongozi wa dini yuko tayari kushirikishwa na uongozi wa chama hicho ili kufanikisha kufikia malengo yanayohitajika.


"Sisi ndio tunaokaa na watu mbalimbali katika shughuli zetu za kila siku hivyo mkihitaji kushirikiana nasi tuko tayari," amesema. 


Pia Askofu wa Kanisa la Uamsho la Morovian, Emaus Mwamakula amesema kuwa wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali katika vyama vya Siasa jambo ambalo linatafsiriwa tofauti na baadhi ya watu.


Amefafanua kuwa kuonekana kwao katika shughuli za kisiasa na kiserikali, kubwa linalofanyika kuhakikisha nchi inakuwa salama na si vinginevyo.





No comments:

Post a Comment