DK.MWINYI AZINDUA FURSA ZA UCHIMBAJI MAFUTA NA GESI ZANZIBAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, March 20, 2024

DK.MWINYI AZINDUA FURSA ZA UCHIMBAJI MAFUTA NA GESI ZANZIBAR



NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inapenda kuzialika kampuni zote za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi kushiriki katika duru ya kwanza 


Rais Dk.Mwinyi amewakikishia wawekezaji wote  wa sekta ya mafuta na gesi kuwa Serikali iko tayari kuwahikikishia mazingira mazuri ya uwekezaji kwa manufaa ya wote.


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo, Machi 20, 2024 mjini Zanzibar wakati akizindua duru ya kwanza ya utoaji wa vitalu kwa kampuni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia maeneo ya baharini. 


Aidha  Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa dhamira ya Serikali katika uchumi wa buluu ni kuimarisha uchumi wa nchi kwa haraka na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo endelevu ya vyanzo vya nishati ya uhakika.


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inaamini kuwa uchumi wa Buluu una fursa nyingi za kukuza mipango ya maendeleo ya kiuchumi yenye lengo la kupunguza umasikini na kutengeneza fursa za ajira nchini.

No comments:

Post a Comment