NA MAGENDELA HAMISI
DUKA la kuuza simu za mkononi la Mandasi Store, limezinduliwa pembezoni mwa kituo cha daladala cha Banana, Gongolamboto jijini Dar es Salaam na wananchi wametakiwa kufika dukani hapo kwa ajili ya kununua ama kupata simu kwa njia ya mkopo kwa gharana nafuu.
Akizungumza wakati wa akizindua duka hilo leo Mei 2, 2024 katika viunga vya Banana, Gongolamboto jijini Dar es Salaam Meya, Omari Kumbilamoto, amesema wananchi hususani wanaotokea Chanika na maeneo ya jirani wataweza kununua ama kukopa simu kwa bei ya chini tofauti na maduka mengine wafikapo dukani hapo.
“Tunakushukuru sana Mkurugenzi wa duka hili, Abdillah Mandasi kwa kusogeza huduma ya ununuzi wa simu ama kukopa kwa gharama nafuu kwa wananchi wetu wa maeneo haya na kinatotakiwa ni kwa mwananchi kufika na kitambulisho cha taifa ili kufikia vigezo vya kukopeshwa simu”, amesema.
Pia Meya Kumbilamoto amemshukuru Mandasi kwa kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 36 wanaotoa huduma ya uuzaji wa simu katika maduka ya Mandasi Store yalipo katika mikoa zaidi ya 11 ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Njombe, Mwanza, Kigoma, Arusha Shinyanga, Iringa na kwingineko.
Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassani, amefungua nchi kimataifa katika suala zima la uwekezaji na wanachofanya Mandasi Store kwa kutoa fursa ya wananchi kupata simu kwa njia ya mkopo ndicho kinachofanywa na nchi kama Dubai, China na nyingezo ambapo wengi wa wananchi hawanunui simu kwa cash.
Aidha amemsisitiza Mkurugenzi huyo, kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ili kujiendeleza kibiashara inayofanikisha kutoa ajira kwa watanzania na kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana na kumuahidi kumpa ushirikiano ili kutimiza ndoto ya kufanya vema katika eneo la uwekezaji.
Naye, Mkurugenzi wa Mandasi Store, Abdillah Mandasi amesema wameamua kutumia vema fursa iliyotolewa na Serikali kupitia kwa Waziri Nape Nnauye alipokuwa Rukwa miaka kadhaa iliyopita alipohitaji watanzania wengi wakopeshwe simu aina ya smartphone ili kuendana na hatua za kidigitali.
“Hadi sasa tayari tumekopesha wananchi 26,000 simu aina ya smartphone na wanaendelea kurejesha kidogokidogo na ninaamini kufungua duka hapa Banana nalo litatoa fursa kwa wakazi wa eneo hili na jirani kuja kwa wingi kupata simu za mkopo kulingana na mahitaji yao na zinapatikana kwa gharama nafuu kabisa,” amesema.
Ameongeza rejesho la chini kabisa mkopaji anaweza kurejesha shilingi 9000 kwa wiki jambo ambalo ni rahisi kwa mtu mwenye kipato cha chini kuweza kumiliki simu ya smartphone na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika duka hilo la Mandasi Store lililopo Banana kituo cha basi wakiwa na kitambulisho cha Taifa.
Mshehereshaji wa tukio hilo, Twarib Omari 'Muwa', ambaye ni Mtangazaji wa kipindi cha Michezo katika kituo cha EFM Radio, akizungumza katika uzinduzi huo.
Wananchi wakifuatilia uzinduzi huo
Mkurugenzi wa duka hilo, Abdillah Mandasi akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto.
No comments:
Post a Comment