NA MWANDISHI WETU
NYOTA wa Hollywood @sydney_sweeney ambaye alipata umaarufu wake kwa mara ya kwanza mnamo 2018 kwenye filamu ya “Everything Sucks” na “The Handmaid’s Tale” yupo nchini Tanzania akifurahia mapumziko @serengeti_national_park hali iliyowatamanisha mastaa wenzake kama @parishilton na @jessicaalba na kucomment kwenye page zake.
Muigizaji huyo mwenye wafuasi zaidi ya milioni 24 katika mtandao wake wa instagram amehusika pia katika filamu iliyoongozwa na Quentin Tarantino inayoitwa “Once Upon a Time”, huko Hollywood.
Mwaka 2024, aliigiza katika filamu ya kishujaa iliyopata umaarufu mkubwa ya “Madame Web”, na hivi karibuni akatayarisha na kuigiza katika filamu ya kutisha ya “Immaculate”.
Muigizaji hiyo amepost katika mitandao yake akionesha kufurahia mandhari za Serengeti ambapo mpaka sasa post hizo tayari zimeangaliwa na watu zaidi ya milioni 5 na kusambazwa zaidi na watu zaidi ya laki 2.






No comments:
Post a Comment