VIJANA WAITWA CHUO CHA FURAHIKA KUSOMA BURE ELIMU YA UFUNDI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, March 14, 2025

VIJANA WAITWA CHUO CHA FURAHIKA KUSOMA BURE ELIMU YA UFUNDI


NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta - Furahika, ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam, umeendelea kuwasisitiza wazazi kutumia nafasi ya programu ya elimu bure kwa kuwapeleka vijana wao kusoma fani mbalimbali bila malipo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya, amesema fursa hiyo ni ya kipekee, hivyo vijana wasipoteze muda mtaani bila kuwa na shughuli ya kufanya waende chuoni hapo kupata ujuzi, bure ili kujitengezea njia mpya ya mafanikio katika maisha yao.

“Hiki chuo ni pekee hapa Tanzania kinachotoa elimu bure kwa vijana na wanacholipia ni ada ya mtihani tu ambayo ni shilingi 50,000 na lengo ni kuunga mkono juhudi ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Rais Samia Suluhu Hassan, kutimiza ndoto za vijana kupitia elimu ya Amali,” amesema.



Pia amesema bado wanaendelea na udahili wa wanafunzi ili wajiunge na muhula mpya kwa kozi za miezi mitatu, sita na mwaka mmoja na baada ya hapo wengi wao watatafutiwa kazi kulingana na kozi ambayo amechukua.

Ameweka wazi kwamba wapo baadhi ya wasichana wanakwenda kufanya kazi za ndani nje ya nchi kutokana na kukosa fursa nyumbani, hivyo ikiwa kijana hususan msichana atajiunga na chuo hicho atafungua njia ya mafanikio katika maisha yake.

Dkt Msuya ametaja kozi zinazofundishwa chuoni hapo ni ‘Nurser Teaching’ ikiwa katika mgawanyo wa Ethics in Professionalism, Teaching methodology, Teaching Practice, Philosophy, Psychology, Children Literature, Communication skills, Early Childhood Education , School Management na First Aid in Schools.

‘Secretarial Course’ ni nyingineyo ambayo inafundishwa na chuo hicho ikigawanyika katika ‘Shorthand, Hatimkato, Office Practice, Secretarial Duty, Typing Skillls, Computer Applicant, Business English na Communication Skillis.



Nyingine ni Passengers Bus Services inayojumuisha Road Safety and Traffic Rules, Customer Care and Communication Skillis, Internet and Emails, Transportation law na First Aid.

Ameongeza kuwa kozi nyingine ni Computer Application, Business Administration yenye vipengere kama vile Introduction Business Management, Communication Skills, Computer Application in Business, Principles of Accounting and bookkeeping, Entrepreneurship, Marketing and Sales Management na Human Resource Management.

Pia amesema kozi nyingine wanazofundisha ni Accounting and Finance iliyo katika mgawanyo wa Introduction of Accounting, Financial Accounting, Business Mathematics na Statistics, Computerized Accounting  System, Taxation and Revenue Management, Entrepreneurship.

Naye mdau wa chuo hicho, Madaraka Omari ‘Bi Kauthar’ amesisitiza wazazi kupeleka vijana wao katika chuo hicho ambacho ni mkombozi kwa vijana wa kitanzania ambao wanachangamoto ya kuendelea na masomo kwa ukosefu wa ada.

No comments:

Post a Comment