NISHATI SAFI YA KUPIKIA SIO GESI NA UMEME PEKEE - MLAY - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, August 30, 2025

NISHATI SAFI YA KUPIKIA SIO GESI NA UMEME PEKEE - MLAY


NA MWANDISHI WETU 

MKURUGENZI wa Nishati safi ya kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay amesema kuwa nishati safi ya kupikia sio gesi na umeme pekee bali ni zaidi ambapo ameeleza uwepo wa kuni smart,pamoja na teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kupikia.


 Ameeleza hayo wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha Kuni Smart cha Chabri Energy Company Limited kilichopo Kijiji cha Kitumba,kitongoji cha Kisha,Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu, jijini Mwanza Agosti 29, 2025.


Aidha, ameeleza kuwa kumekua na dhana katika jamii kuamini kuwa nishati safi ya kupikia ni gesi na umeme pekee lakini ukweli ni kuwa nishati safi ya kupikia ni pamoja na mkaa safi (Kuni Smart) ambao unatengenezwa katika kiwanda hiki kwa kutumia mabaki ya mbao.


Vilevile, Mlay ameeleza kuwa nishati safi ya kupikia ni fursa ambayo inawainua wananchi kiuchumi pamoja na kukuza uwekezaji kama huu ambao umefanywa na Chabri Energy Company Limited ambao umekua njia ya kufungua fursa za kuajiri vijana ambao wanaendesha maisha yao kupitia uwepo wa kiwanda hiki.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Chabri, Bernard Makachia ameeleza kuwa mahitaji ya bidhaa wanazozalisha katika kampuni yao yamekua kwa kiasi kikubwa kutokana na uelewa wa jamii kuhusu uwepo wa kuni Smart.


Vilevile Makachia aliendelea kusisitiza kuwa kumekuwa na dhana kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuamini kuwa gesi na umeme pekee ndizo nishati safi za kupikia.


Makachia ameeleza kuwa kampuni ya Chabri imekua ikitoa huduma katika shule takribani 50 na baadhi ya magereza yaliyopo katika ukanda huu.


Ameeleza kuwa Ubunifu huu wa kutengeneza kuni smart umeongeza fursa kwa wananchi kuweza kutambua nishati safi ya kupikia pamoja na kupunguza gharama ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia kuni Smart ambazo gharama yake ni nafuu.





No comments:

Post a Comment