DKT. BITEKO ASEMA DKT. NCHIMBI NI CHAGUO SAHIHI NA MWALIMU WA WENGI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 6, 2025

DKT. BITEKO ASEMA DKT. NCHIMBI NI CHAGUO SAHIHI NA MWALIMU WA WENGI


NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA  wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa  Chama Cha Mapinduzi kimepata Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais, anayefaa na kujua majukumu yake ambaye ni Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi.


Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 6, 2025  wakati  akiwasalimia wananchi wa Katoro kwenye Kampeni za Mgombea Mwenza wa nafasi ya hiyo ya Urais kupitia CCM, Balozi. Dkt. Nchimbi.


“ Tumepata Mgombea Mwenza anayejua kazi, anayejua shida za watu yeye ni mwalimu wa wengi nikiwemo mimi ametufundisha mengi,” amesema Dkt. Biteko


Ameendelea kubainisha sifa za Dkt. Nchimbi na kusema kuwa ni mtu mwema anayejua kumuweka karibu kila mtu na ambaye hazungumzii wapinzani katika hotuba yake ispokuwa CCM, kazi yake na kubadilisha maisha wa wananchi.


Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo, Dkt. Biteko amewaeleza wananchi wa Katoro na Geita  kuwa Uchaguzi na kura yao ni maisha yao hivyo amewaomba Oktoba 29 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kupiga kura.



Amesisitiza “ Najua Katoro hamna mbambamba, kwenu nyie hamna mechi ndogo hata mazoezi kwenu nyie mechi, nawaomba mtuchagulie madiwani na mbunge ili waungane na Dkt. Samia Suluhu Hassan ili tuweze kuleta maendeleo ya Katoro na Katoro lazima ibadilike,”


Aidha, amesema Geita inawaunga mkono Dkt. Samia na Nchimbi, wabunge na madiwani wa CCM na inahusisha Uchaguzi na maisha yao  hivyo wanachagua kwa ajili ya maisha yao.


No comments:

Post a Comment