MAKINI KUMPA AJIRA DKT SAMIA IKIWA WATAFANIKIWA KUINGIA IKULU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, September 3, 2025

MAKINI KUMPA AJIRA DKT SAMIA IKIWA WATAFANIKIWA KUINGIA IKULU


NA MWANDISHI WETU


MGOMBEA Urais kupitia Chama Makini, Coster Kibonde akiwa atachaguliws kuwa Rais katika uchaguzi Mkuu ujao atasimia vipaumbele vitatu ili kuleta maendeleo Kwa Watanzania .


Amesema hayo leo Septemba 2, 2025 katika viwanja vya Manzese Bakheresa jijini Dar es Salaam wakati akizundua kampeni za chama chake kuelekea uchaguzi utakaifanyika Oktoba 29 mwaka huu.


Vipaumbele ambayo ataanza navyo ni Elimu ambapo itatolewa Bure kuanzia elimu ya awali, Sekondari hadi Chuo Kikuu.


Pia amedadavua kuwa kipaumbele kingine ni Kilimo ambapo atatoa ekari tano Kwa kijana wa kitanzania pamoja na kugawa pembejeo zitakazotokana na viwanda vya ndani.


Pia akifanikiwa kuwa Rais, atajenga zahanati kila Kata zitakazokuwa na madaktari na vifaa tiba ili kutoa hudumu ya uhakika kwa wagonjwa.


Mgombea huyo pia amesema ikiwa ataingia Ikulu atampa ajira mgombea urais kupitia chama Cha Mapinduzi CCM, kutokana na uzoefu alionaka katika masula ya Kimataifa.




"Nikifanikiwa kuingia Ikuru, mgombea urais kupitia CCM, DKT Samia Suluhu Hassan, nimbakisha katika viunga vya Ikulu kutokana na kuwa mzoefu wa masuala mbalimbali ya kimataifa, hivyo nawaomba watanzania wanichague Kwa kishindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.


"Pia  wananchi watakaponipa ridhaa na tume huru kunitangaza kuwa Rais wa nchi hii viongozi wote walioingia kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya urais nitawapa nafasi kwenye serikali yangu lakini nafasi ya kwanza nitampa Dkt Samia Suluhu Hassan kwani huyu ni mwana diplomasia mzuri na ninaamini atakwenda kuifanya kazi nzuri kwenye serikali, "amesema.

Ameongeza kuwa pindi watakapofanikiwa kuingia Ikulu, watatoa pikipiki1,000,000 bure kwa vijana lengo ni kuchochea ajira na  kutoa mkopo wa milioni 10 kwa kila mfanyabiashara wa mitumba pamoja na kutoa posho ya laki moja kwa mwezi kwa wazee nchi nzima.

Wakati huo huo ameipongeza Tume huru ya uchaguzi (INEC) kwa kuvishirikisha vyama vya siasa katika kila hatua na kuwapitisha kwenye sheria zote hivyo imewapa inami ya kuwa na uchaguzi huru na haki.

No comments:

Post a Comment