MCHANGE: KUZUIA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI NI KUUA DEMOKRASIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 23, 2025

MCHANGE: KUZUIA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI NI KUUA DEMOKRASIA


NA MWANDISHI WETU 


Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) kimekemea vikali tabia za baadhi ya vyama vya siasa kuwalazimisha wananchi kususia uchaguzi ni kuwanyima  haki ya msingi kwa mujibu wa katiba.


Chama husika hakishiriki uchaguzi  hatua hiyo ambapo ni  kinyume cha demokrasia ya kutaka kufanya  jaribio la kupora haki za wananchi. 


Mwenyekiti wa MECIRA, Mchange Habibu, akizungumza leo katika kipindi cha Kipindi cha Wasafi  Good  Morning amesema kwa kusisitiza kuwa   Demokrasia inasimama juu ya misingi ya uhuru wa mtu mmoja mmoja kufanya maamuzi kwa hiari yake.


“Kila raia ana haki ya kushiriki au kutoshiriki uchaguzi kwa hiari yake. Hii ni haki ya kikatiba isiyoweza kufutwa na chama chochote. Chama kinaweza kususia, lakini haki ya wananchi kushiriki inabaki palepale. Demokrasia halisi inajengwa kwa hoja na heshima, si kwa shinikizo,” alisema.


Amesema wito wa MECIRA kwa Wananchi ni kuhamasisha wananchi wasikubali kulazimishwa juu ya kutopiga kura kwani ni haki yao ya kikatiba na sehemu ya maamuzi ya kuliendea jambo hilo la kupiga kura


Amesema kila kura ni inayipigwa na mwananchi ni  sauti yake katika kuja kudai maendeleo kwa kiongozi aliyemchagua na sio mtu ambaye alisusia uchaguzi.


Mchange amesema demokrasia ni uhuru na siyo amri ya kushinikizwa na chama cha siasa ambacho hakijashiriki uchaguzi .



MECIRA imeongeza kuwa mfumo wa vyama vingi unalindwa na Katiba, hivyo hata chama kimoja kisiposhiriki, vyama vingine vinabaki na nafasi ya kushindana kwa mujibu wa sheria.


 “Kususia ni mtazamo wa chama fulani, lakini kuwalazimisha raia wote kufuata msimamo huo ni kuua roho ya demokrasia. Kura yako ni thamani yako,” amesema  Mchange.

No comments:

Post a Comment