MWANDISHI WETU
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Richard Lyimo ikiwa atapata ridhaa ya kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu ujao atafungua viwanda kwa ajili ya kuinua maisha ya Watanzania hususan vijana.
Pia vikindi mbalimbali vya vijana vilivyopo katika uwekezaji vitaimarishwa ili kuinua uchumi wa kundi hilo ambalo wengi wao wamekuwa hawana ajira na kuwa tegemezi kwa jamii hususan familia za.
Ameyasema hayo, leo Septemba 4, Manzese jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.
"Tutawafungulia viwanda vijana watazalisha mali na vikundi vyote vya vijana vitaimarishwa ili kuchochea maendeleo ya kundi hili ambalo ni uti wa mgongo wa Serikali", amesema.
Pia amesema vipaumbele vingine watakavyovisamia ni Elimu ambapo itatolewa bure kuanzia ya awali hadi Chuo Kikuu na kunatakuwa na madarasa ya ufundi ili kuzalisha wataalam
Pia amesema suala la Afya Kwa watanzania, kila mwananchi atapewa bima ya matibabu.
Naye Mwenyekiti wa Wanawake Taifa na Mgombea Jimbo la Ilala, Nuru Mwandila amesema Tanzania ina rasirimali za kutosha hivyo kupitia sera ya chama chao ikiwa watafanikiwa kushika Dola kuna uwezekano wa kumpa kila Mtanzania Shilingi milioni 1 za mtaji.
"Watanzania wanapaswa kupewa elimu na fedha za mitaji tupeni kura twende tukarekebishe haya , tunahitaji keki ya taifa tugawane wote," amesema.
Naye Makamu Mwenyekiti Taifa wa TLP, Johari Rashid amesema ikiwa watakuwa washindi katika uchaguzi Mkuu ujao, watakwenda kusimamia vipaumbele vyao kwa uhakikika kwa maslahi ya wananchi
No comments:
Post a Comment