![]() |
NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR
WITO umetolewa kwa vijana kujitokeza kwa wingi kujiunga na Chuo cha Zanzibar Islamic kwa ajili ya mfunzo ya Amali yatakayowawezesha kujitegemea na kujiendeleza kimaisha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Akira na Uwezeshaji Zanzibar, Khalid Waziri ametoa wito huo leo Mei 9, 2026 wakati wa mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika Darajani Unguja kisiwani Zanzibar.
"Hiki chuo cha Zanzibar Islamic kilichopo hapa Darajani kinatoa mafunzo ya Amali bure kwa waliomaliza kidato cha nne, darasa la Saba na walioshindwa kuendelea na masomo, hivyo nawaomba vijana wa kike na kiume mje kusoma hapa ili mjikomboe kimaisha.
Kwa maana elimu ya amali ndio msingi sahihi wa kuondokana na umasikini kwa maana itawafanya kuingia kwenye soko la ajira moja kwa moja na kuachana na utegemezi ,"amesema
.jpg)





No comments:
Post a Comment