NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI wa Maendeleo ya Vijana Tanzania, Dk David Msuya ametoa wito kwa Serikali kutunga sheria maalumu zitakazowazuia wanafunzi kwenda kufanya kazi za ndani kwenye nyumba za walimu au kupeleka mizigo.
Dk.Msuya amezungunza hayo leo Juni 3, 2026 na kusisitiza kwamba wanafunzi wanapaswa kulindwa dhidi ya vitendo vinavyoweza kuathiri haki zao za kupata elimu na maendeleo yao.
"Zipo kesi kadhaa ambazo baadhi ya walimu kuwanyanyasa kingono wanafunzi wao na hatua zimeshindwa kuchukukiwa kutokana na wazazi kulaghaiwa kimaslahi na haki kishindwa kutendeka Kwa kukosekana Kwa ushahidi mahakamani, hivyo ni vizuri sheria zikaundwa ili kudhibiti walimu kuwatumia wanafunzi kufanyakazi majumbani mwao.
Pia hata kipindi hiking amnacho tunaiomba Serikali kutunga sheria pia maofisa elimu kuanzia ngazi ya Kata hadi Mkoa nao wakalikemea jambo hili ili kulinda haki ya mwanafunzi.," amesema.
Amesisitiza kuwa mazingira ya shule yanapaswa kuwa salama na yenye kuzingatia maadili ya kitaaluma, huku akitaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya walimu watakaobainika kuwatumia wanafunzi kwa shughuli zisizohusiana na masomo.
Ameongeza kuwa mwanafunzi anapotolewa darasani kwenda kufanya kazi za ndani kwa mwalimu hiyo si sawa kwani vipindi vya darasani vinampita na haki ya msingi iliyofanya aende shule nayo anaikosa.





No comments:
Post a Comment