NGORONGORO NI NYUMBANI-WABUNGE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, June 28, 2026

NGORONGORO NI NYUMBANI-WABUNGE


WABUNGEB wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)kutoka Zanzibar wametembelea hifadhi ya Ngorongoro na kustaajabishwa na historia  ya binadamu, malikale, Urithi wa Utamaduni na Wanyamapori na kutoa wito kwa watu mbalimbali kutembelea hifadhi hiyo yenye hadhi tatu za Kimataifa zinazotambuliwa na UNESCO 


Akizungumza kwa niaba ya wabunge hao mbunge wa viti maalum Mhe. Zainab Abdallah   ameeleza kuwa katika ziara hiyo wameshuhudia maendeleo yaliyotukuka kuhusu uhifadhi, utalii, Malikale, urithi wa utamaduni na maendeleo ya jamii ambapo vinadhihirisha  kuwa Ngorongoro ni kivutio bora cha Utalii Barani Afrika.


“Kuona ni kuamini, jana na leo tumetembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro na tumeona maendeleo makubwa yakifanyika na kwa macho yetu tumeshuhudia idadi kubwa ya watalii waliojawa na nyuso za bashasha na furaha kwa kushuhudia vivutio vilivyopo, mandhari na hali ya hewa ambayo unaipata Ngorongoro pekee”,amesema Mhe. Zainab.


Wabunge katika ziara hiyo walielezwa kuhusiana na historia ya kutokea kwa kreta ya Ngorongoro, chimboko la binadamu wa kale na namna ambavyo mabadiliko ya viumbe mbalimbali yanavyoendelea kutokea kwa nyakati tofauti.


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Idara ya maendeleo ya jamii, Gloria Bideberi akizungumza kwa niaba ya kamishna  wa Uhifadhi Ngorongoro, Abdul-Razaq   Badru amewapongeza wabunge hao kwa kufanya maamuzi sahihi ya kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali na kuwaomba kuendelea kuwa mabalozi wa kuitangaza Ngorongoro ambayo imepata tuzo ya kuwa chaguo la Wasafiri(Watalii) la kiwango cha Juu cha Ubora mwaka 2026 (Travellers Choice Awards, Best of the best 2026)


Eneo la hifadhi ya Ngorongoro linasifika duniani kutokana na kuwa na ikolojia yenye mchanganyiko wa viumbe mbalimbali kuishi kwa pamoja Ngorongoro kwa miaka mingi.






No comments:

Post a Comment