WATANZANIA WAHIMIZWA KUDUMISHA AMANI, UTULIVU WA TAIFA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, June 4, 2026

WATANZANIA WAHIMIZWA KUDUMISHA AMANI, UTULIVU WA TAIFA


NA MWANDISHI WETU


WATANZANIA wameaswa kuacha kusikiliza wanaharakati na wanasiasa wanaochochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini, kwa kuwa watu hao hawana nia njema kwa taifa.


Rai hiyo ilitolewa, Juni 4, 2026, jijini Dar es Salaam na mwanafalsafa wa Pan-Afrika kutoka Zimbabwe, Dk. Joshua Maponga, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliohusu uzinduzi wa makala inayozungumzia matukio yaliyojitokeza kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.


Dk. Maponga amesema kuwa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yamekuwa yakipokea fedha kutoka mataifa ya nje kwa lengo la kuhamasisha vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili na amani ya nchi, ikiwemo vurugu na migawanyiko kati ya wananchi na viongozi wao.


Amesema hali hiyo ni hatari kwa ustawi na usalama wa taifa, hivyo akashauri Serikali kuchukua hatua za kufanya uhakiki wa mashirika hayo ili kubaini vyanzo vya fedha wanazopata na namna zinavyotumika.


Aidha, ameeleza kuwa watu wanaochochea vurugu mara nyingi huishi nje ya nchi katika mazingira mazuri, huku wananchi wanaoshiriki machafuko hayo wakikabiliwa na madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha, mali na makazi yao.


Dk. Maponga pia aliwataka waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu athari za maandamano yasiyo ya amani na vurugu, akisisitiza kuwa matukio hayo yanaweza kuathiri maendeleo na rasilimali za taifa.

No comments:

Post a Comment