NA MWANDISHI WETU
WACHEZAJI 12 wa Timu ya Taifa ya Tanzania wanaokwenda kushiriki Michezo ya Jumuia ya Madola nchini Scotland wameagqa leo jijinj Dar es Salaam.
Neema Msita, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), amewataka wachezaji hao kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ili kuvuka rekodi iliyowekwa na timu ya Tanzania katika mashindano yaliyopita.
"Wenzanu katika mashindano yalipita medali tatu, sasa mnachotakiwa ni kwenda kufanya vizuri ili mvuke rekodi hiyo mtakuwa na wakati mgumu ikiwa mtarudi bila medali yoyote itaonekana kama 'tulibeep'," amesema.
Pia Msita aliwashukuru viongozi Vyama vya Michezo kwa kufanikisha kuandaa mashindano mbalimbali yaliyofanikisha kupata timu hiyo.
Aidha aliwashukuru makocha ambao wamefanikisha wachezaji hao kuwa tayari kushiriki mashindano hayo yanayoanza Julai 23 hadi Agosti 2 mwaka huu.
Naye kiongozi wa msafara huo,Henri Tandau amebainisha kuwa kwa mara ya Tanzania inapeleka bondia wa kike ambaye ni Zawadi Mutaka.
"Naaminj bondia wetu wa kike atakwenda kufanya vizuri ili kujiweka kwenye ramani kimataifa, pia amewataka wanamichezo hao Kwa ujumla kwenda kujipambania wenyewe kwa maslahi ya nchi," amesema.
Pia nahodha wa timu hiyo, Cornel Saliboko ameahidi kikosi kufanya vizuri na kurejea na medali na kuishukuru Serikali Kwa sapoti kuanzia maandalizi posho za wachezaji hadi safari.
Katika mashindano hayo Tanzania imewakilishwa na timu ya Nguni, Kuogelea, Riadha na Mieleka.








No comments:
Post a Comment