KAMPUNI YA UHANDISI YA ROWAD MODER YA MISRI YATEMBELEA TARURA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, August 5, 2026

KAMPUNI YA UHANDISI YA ROWAD MODER YA MISRI YATEMBELEA TARURA


NA MWANDISHI WETU, DODOMA


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) leo tarehe 5 Agosti, 2026 imepokea ujumbe kutoka Kampuni ya Uhandisi ya ROWAD MODERN ENGINEERING ya nchini Misri kwa lengo la kufanya majadiliano kuhusu fursa za ushirikiano na uwekezaji katika miradi ya ujenzi na maendeleo ya miundombinu ya barabara nchini.


Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Makao Makuu ya TARURA, Mtumba jijini Dodoma, yaliongozwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Edward Amboka huku ujumbe wa ROWAD MODERN Engineering ukiongozwa na Ahmad El Zeny.


Ziara hiyo inaashiria kuendelea kuimarika kwa mahusiano ya kimkakati kati ya TARURA na wadau wa kimataifa ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuvutia uwekezaji na kuongeza ubora wa miundombinu ya barabara za vijijini na mijini ili kuchochea maendeleo endelevu.





No comments:

Post a Comment