KATAMBI ASAINI KANUNI KUDHIBITI VING’ORA BARABARANI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, September 3, 2026

KATAMBI ASAINI KANUNI KUDHIBITI VING’ORA BARABARANI

 


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesaini Kanuni za ving'ora, Ishara zinazosikika na vimulimuli za  mwaka 2026  ili kudhibiti matumizi ya sauti katika vyombo vya usafiri.


Katambi amesema hayo leo mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM), ambako amewasili leo kwa ziara ya kikazi.


“Kila mtu amekua na king’ora kwa hiyo imekua familia ya kambare,ukinunua gari yako unaweka king’ora,bodaboda ina king’ora sasa shughuli hazitaenda ikiwa kila sehemu ni ving’ora tu,sasa ving’ora vitatumika kwa utaratibu maalumu unaotambuliwa na sheria”amesema Waziri Katambi

No comments:

Post a Comment