NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba amesema kwamba thamani ya mfuko huo imeongezeka na imefika Shilingi trilioni 11.47.
Ameongeza kuwa pia Uwekezaji wamfuko huo nao umeongezeka kutoka Shilingi trilioni 4.6 Juni 2021 hadi zaidi ya Shilingi trilioni 9.6 Juni 2026.
Mshomba amesema hayo keo, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari katika kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Pia amefafua kwamba ukuaji wa mfuko umeenda sambamba na ongezeko la malipo ya mafao kwa wanachama na wategemezi wao.
Amesema,NSSF ililipa takribani Shilingi bilioni 594 katika kipindi cha mwanzo cha mpango uliopita, lakini kiasi hicho kiliongezeka hadi zaidi ya Shilingi trilioni 1.16 katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Amesema, ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa idadi ya wanachama wanaofikia vigezo vya kupata mafao mbalimbali, ikiwemo pensheni ya uzeeni, pamoja na mafao mengine yanayotolewa kwa mujibu wa sheria."
Pia amefafanua kwamba
mafanikio yaliyopatikana katika mpango uliopita, mfuko huo umekuwa ukiongeza wanachama, makusanyanyo, uwekezaji na malipo ya mafao.
Amesema, idadi ya wanachama iliongezeka kutoka 1,392,112 katika kipindi cha mwanzo cha mpango uliopita hadi zaidi ya milioni 2.1 kufikia Juni,2026.
Amesema, ongezeko hilo lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, pamoja na hatua zilizochukuliwa na NSSF katika kuimarisha ukaguzi, uhusiano na waajiri na matumizi ya teknolojia.
Kwa upande wa makusanyo, Mshomba amesema, NSSF ilikusanya zaidi ya Shilingi trilioni 1.17 katika mwaka wa mwanzo wa mpango huo, kabla ya kufikia Shilingi trilioni 2.90 katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Amesema, hatua hiyo inaonesha ongezeko kubwa la mapato ya michango ya wanachama katika kipindi hicho.
Katika ukusamyaji mapato kutoka kwa waajiri ameweka wazi hawamuogopi mwajiri yeyote na ikawa mhusika atashindwa kulipa michango kwa wakati hatua ya mwisho n kumfikisha mahakamani huku akiwatikiwa kabla ya kesi kusikilizwa kulipa asilimia 50 ya kiasi cha michango anachotakiwa kulipa.
"Waajiri ni vema sasa wakaendelea na utaratibu wa kulipa michango wakati ili kuondoa mivutano isiyokuwa na msingi na tutaendelea kusimamia sheria zetu ili kuhakikisha kila jambo linakaa katika mstari wake," amesema.
Mkurugenzi huyo, amesema mikakati yao ni kuhakikisha ifikapo Juni 2031 thamani ya mfuko ifikie trilioni 24.75 pamoja na kuongeza wanachama.








No comments:
Post a Comment