MPANGO WA MIAKA MITANO NGORONGORO NI DIRA YA KULINDA UHAI WA HIFADHI: JENERALI MABEYO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 28, 2026

MPANGO WA MIAKA MITANO NGORONGORO NI DIRA YA KULINDA UHAI WA HIFADHI: JENERALI MABEYO


NA MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuandaa mpango mkakati wa shirika (CSP)  wa miaka  5 na mpango wa muda mrefu  (LTTP) wa miaka 25 kwa kuzingatia maslahi makubwa ya uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.


Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo katika kikao cha bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka hiyo kinachoendelea jijini Arusha kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za shirika kwa robo ya kwanza kuanzia mwezi Julai hadi septemba katika mwaka wa fedha 2026/2027


Ameeleza kuwa uhifadhi na ikolojia ya Ngorongoro na pori la akiba la Pololeti ni lazima ilindwe kwa nguvu zote kwa kuwa uwepo wake unachangia uhai wa hifadhi nyingine ambapo kwa pamoja huchangia kuongeza na kulinda ajira za watanzania na kupata mapato ya Serikali kupitia wageni wanaotembelea ambapo mapato hayo husaidia kuboresha huduma za jamii na maendeleo ya nchi. 


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru amesema mpango wa shirika hilo umezingatia nyaraka na miongozo mbalimbali ya serikali kupitia dira ya taifa ya 2025-2050 na ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2025-2030.





No comments:

Post a Comment