Na Mwandishi Wetu, Mwanza
RICHARD Laizer wa Arusha ameibuka na ushindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle Challenge, baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya 400 kwa upande wa wanaume.
Kutokana na ushindi huo, amejinyakulia zawadi ya sh 1,500,000 na kuvikwa taji lililokuwa likishikiliwa na Hamis Clement wa Shinyanga, baada ya kutumia muda wa saa 5:02:28 kumaliza mbio hizo za kilometa 196.
Mshindi wa pili wa michuano hiyo kwa wanaume ni Mindi Mwagi wa Shinyanga aliyetumia saa 5:02:29, ambaye amezawadiwa sh 1,000,000, akifutiwa na Said Jumanne wa Arusha aliyezawadiwa sh 700,000.
Kwa upande wa wanawake, Mkoa wa Arusha uliibuka kidedea baada ya mshiriki wake, Sophia Hussein kuwabwaga washiriki wenzake zaidi ya zaidi 60 na kunyakua nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ya kilometa 80 akutumia muda wa saa 2:25:13.
Kwa ushindi huo, Sophia amejishindia kitita cha sh 1,100,000 na kushikilia taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Sophia Adison wa Arusha, huku akifuatiwa na Mwajuma Musa kutoka Arusha aliyetumia saa 2:25:40 na kujinyakulia zawadi ya sh 800,000.
Hata hivyo, Mkoa wa Shinyanga nao haukuwa nyuma katika mashindano hayo baada ya Salome Donard kushika nafasi ya tatu, ambapo alizawadiwa kiasi cha sh 600,000 baada ya kutumia saa 2:26:21 kuhitimisha mbio hizo za kilometa 80 kwa wanawake.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa, Steven Kingu, ambae ndiye alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza washiriki wote hususani washindi na kuahidi kwamba kampuni yake itaendelea kuratibu na kuandaa michuano hiyo ili kuifanya kuwa ya kimataifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), Ephraim Mafuru ambao ni wadhamini wenza kupitia kinywaji kisicho na kilevi cha Malta Guinness, alisema hawajutii kudhamini michuano hiyo kutokana na hadhi iliyonayo.
Monday, October 24, 2011
New
Vodacom Mwanza Open Cycle Challenge 2011 yafana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment