Nchimbi kuhudhuria tamasha la makabila - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, October 24, 2011

Nchimbi kuhudhuria tamasha la makabila

Nchimbi kuhudhuria tamasha la makabila
Na Asmah Mokiwa
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la utamaduni wetu na muziki wa kizazi kipya litakalofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Novemba 11 hadi 12.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa tamasha hilo, Ismail Mnikite alisema lengo la tamasha hilo ni kuangalia tofauti iliyopo kati ya muziki wa asili na wa kizazi kipya.
Alisema tamasha hilo pia litawapa nafasi wasanii hao kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya sanaa.
Mnikite alisema kuwa vikundi vitano vya ngoma za asili pamoja na wasanii wa Bongo Fleva watatumbuiza katika tamasha hilo.
Makabila hayo ambayo yatatumbuiza ni pamoja na Wamasai, Wachaga, Wapare, Wamang'ati na Wamburu, ambayo yote ni makabila ya Arusha na Kilimanjaro.
Wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Mabaga Fresh, Afande Sele, Mandojo na Domokaya, Godzilla na Adam Mchomvu.
Alisema tamasha hilo pia litatumika kudumisha amani kwa waliokoseana wakati wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

No comments:

Post a Comment