Na Hamisi Magendela
MSANII chipukizi wa kundi la Wa Manzese Army, Hamisi Swalehe 'Dilli', anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Hatufanani' Novemba mwaka huu.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Dilli, alisema mashabiki wa muziki wa kizazi kipya watarajie mambo mazuri kutoka kwake kwani amejiandaa vizuri kuonesha uwezo katika tasnia hiyo.
"Ninaachia wimbo mpya ambao naamini utanitambulisha vizuri kwenye ushindani wa muziki japo 'game' linaonekana kuwa na changamoto kubwa, hivyo nimejiweka sawa kuzikabili changamoto zote," alisema Dilli.
Alisema baada ya wimbo huo atafanya kazi za kundi ambazo ziko mbioni kumalizika likiwa chini ya Emanuel Elibariki 'Ney wa Mitego', ambapo muda wowote wataingia studio kukamilisha kazi hizo.
Pia, Dilli aliongeza kuwa wimbo huo umetengenezwa katika studio ya Back Yard, chini ya mtayarishaji Samweli Mbwana 'Bryton', na anaamini kuwa utaweza kushika chati katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na maudhui yake.
Amewaomba mashabiki wa muziki huo kumpokea kwa mikono miwili ili aweze kuonesha uwezo katika ulingo huo wa muziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Bongo Freva.
Monday, October 24, 2011
New
Dilli kuachia mpya Novemba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment