Na Salome Millinga
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Iman Madega amepewa tuzo maalum ya heshima na kuthamini kazi aliyoifanya na Chuo Kikuu cha Dar es Salaan mwishoni mwa wiki iliyopita.
Madega amefikia hatua hiyo katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru katika kitivo cha sheria chuoni hapo, ambapo mwenyekiti huyo amesoma hapo na kupata mafanikio makubwa.
Madega ambaye kwa sasa ni mwanasheria, alipewa tuzo hiyo katika sherehe ambazo zilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Ghalib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba.
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa tuzo hiyo, Madega alisema amejisikia mwenye bahati na furaha na amepata changamoto kubwa kuona kuwa chuo hicho kimetambua mchango wake.
Alisema anaamini kuwa elimu yake aliyoipata chuoni hapo ilikuwa na maana kubwa katika maisha yake na aliweza kusimamia vizuri klabu ya mabingwa hao pamoja na kuwapa ubingwa katika misingi ya kisheria.
"Imekuwa faraja kwangu kuona chuo kimethamini mchango wangu na kuona kuwa nastahili pongezi, hii inaonesha kuwa elimu yangu ya sheria niliyopata hapa imeweza kufanya kazi hata katika michezo na kuiongoza taasisi kubwa kama Yanga," alisema Madega.
Monday, October 24, 2011
New
Chuo Kikuu Mlimani champongeza Madega
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment