Na Asha Kigundula
UONGOZI wa klabu ya Simba umesema hauna mpango wa kuondoa kikosi chake kwenye kambi ya timu hiyo iliyopo Bamba Beach, Kigamboni.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, alisema wao awatahamisha timu kwenda popote kwa kuwa wanajua mchezo wa Yanga ni kama mchezo mwingine katika Ligi Kuu inayoendelea.
Mtawala alisema kuwa timu yake itaendelea kuwepo katika kambi yake hiyo mpaka wamalize mechi zake mbili zilizobaki katika Ligi Kuu.
Alisema mechi yao dhidi ya Yanga ni kama mechi nyingine zilizopita, hivyo hawaoni sababu ya kuhamisha timu kuipeleka mafichono zaidi kwa mchezo kama huo.
"Sisi kambi yetu bado ipo pale pale kwa nini tuhameshe kambi kwa ajili ya mechi moja wakati mecho zote zina umuhimu, zote unaweza kupata pointi tatu kama una nia ya dhati, na hii ni sawa na zile pia," alisema Mtawala.
Wakati huo huo, safari ya timu ya soka ya Yanga kwenda nchini Msumbiji imevunjika, na sasa wameamua kuangalia sehemu nyingine mkoani Pwani.
Habari kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa klabu hiyo ina mpango wa kuweka kambi yake latika kisiwa cha Mafia au Bagamoyo, na si Msumbiji kama ilivyotangaza awali.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema mpaka sasa hajajua wapi kambi ya timu hiyo itawekwa pamoja na kuwepo kwa taarifa tofauti anazozisikia bila kuwa rasmi.
Monday, October 24, 2011
New
Yanga yaghairi kwenda Msumbiji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment