Na Charity James
SHIRIKISHO la Ngumi za Riadha Tanzania (BFT), limesogeza mbele mashindano ya Kombe la Kova hadi Novemba 14 mwaka huu.
Awali, mashindano hayo yalipangwa kufanyika Oktoba 24 hadi 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam, lakini mabadiliko hayo sasa yanaifanya michuano hiyo kupigwa Novemba 14 hadi 18.
Katibu Mkuu wa BTF, Makole Mashaga, alisema kuwa wameamua kusogeza mbele mashindano hayo ili kuwapa nafasi mabondia watakaoshiriki kufanya mazoezi ya nguvu zaidi.
Mashaga alisema wamelenga kupata mabondia wa kuwaongeza katika timu ya taifa, hivyo wameamua kusogeza mbele kwa ajili ya kupata muda wa kujifua zaidi.
Alisema mashindano hayo yatatumika kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika nchini Pakistan baadae mwaka huu, na Tanzania wakiwa waalikwa katika mashindano hayo.
"Tumesogeza mbele mashindano haya ili kuwapa nafasi mabondia kufanya mazoezi kwa lengo la kutusaidia kufanya haki pindi tutakapochagua wachezaji wa kuwaongeza katika timu ya taifa," alisema Mashaga.
Monday, October 24, 2011
New
BFT yasogeza mbele Kova Cup
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment