DKT NJAMA AJITOKEZA KUWANIA JIMBO LA KIBAMBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, June 30, 2025

DKT NJAMA AJITOKEZA KUWANIA JIMBO LA KIBAMBA


NA MWANDISHI WETU


MTUMISHI wa Idara ya Afya katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Dkt Ally Njama, amejitokeza kuchukua fomu ya  kutia nia kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba.


Dkt Njama, historia yake katika kutimiza majukumu ya kichama na Serikali, inaonesha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Aidha kada huyo wa CCM, aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi katika Hospitali ya Mwananyamala kwa miaka minne na aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi wa Shule ya Sekondari Kambangwa iliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Pia ni Mjumbe wa Chama Cha Serikali za Mitaa (TALGU)  na alikuwa Mjumbe wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) akitumikia vipindi vitatu.


Kutokana na uzoefu huo, mwanachama huyo, anakiri kwamba anaweza kuliongoza Jimbo la Kibamba ikiwa jina lake litarejeshwa kuwania nafasi hiyo.




No comments:

Post a Comment