-Awataka wasanii kupendana
-Turudi kijijini yamuweka pazuri
Na Hamisi Magendela
MIONGONI mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini (Bongo Fleva) ambao katika harakati zao za kutafuta
maisha kupitia tasnia hiyo na kupata tabu, uwezi kusita kutaja jina la Nassoro Hamisi 'Best Naso'.
Si jina geni masikioni mwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya hasa kutokana na umahili wake
katika utunzi na upangaliaji wa sauti yake.
Hakika naweza naweza kusema kuwa baada ya kuvuja jasho wakati akianza harakati za kutafuta mweleleo katika
'game' sasa amefikia mahala pa kujivunia kutokana na kuanza kukubalika na jamii ukiachilia mbali mafanikio
aliyonayo hivi sasa.
Best Naso kama anavyofahamika na wengi katika tasnia ya muziki alianza kujikita zaidi katika tasnia ya muziki akiwa Nyumba ya Mungu mkoani Klimanjaro baada ya kuhisi kuwa anakipaji cha kufanya hivyo.
Akiwa katika harakati za kusaka shilingi ili kuendeleza kiu yake ya kuwa mwanamuziki wa kimataifa kama walivyokuwa wengine katika ulingo huo, alikutana na rafiki yake anaeitwa Sila na kukubaliana kufanya kazi
pamoja.
"Tulikubaliana kufanya kazi pamoja katika shughuku za kisanii sanjari na kufanya shughuli nyingine tikiwa na
malengo ya kufungua studio yetu wenyewe kwa kipato tutakachokipata," anasema Best Naso.
Akiwa katika utafutaji wa riziki ili kufikia malengo aliyojiwekea alifanya kazi katika kiwanja cha kutengeza vinu vya mashine cha Babson na kipato walichokipata walinunua baadhi ya vifaa vile Computer, Mixer na vitu vingine vya kufungulia studio.
Penye riziki hapakosi fitina' ni msemo wenye maana kubwa ambao wahenga waliutumia wakiwa na maana kuwa katika sehemu yoyote ya kujipatia riziki machungu na fitina yanakuwepo yakiwa na lengo la kuharibu utendaji kazi.
"Wakati tukiwa na studio yetu ndogo na utendaji wangu kuwa mzuri na vijana wengi wakiwa wananihusudu, mwezangu akanionea chuki na kunifukuza kwao na tukagawana vifaa, nami nikachukua Mixer na kuishi kwa marafiki kutokana na kutokuwa fedha za kutosha
kupanga chumba," alisema Best Naso.
Anasema hiyo haikuishia hapo kwa mwenzake huyo alikwenda polisi na kufumfungulia kesi ya uvunjaji na kupelekwa polisi na kukaa kwa siku kadhaa na baadhi ya watu alikokuwa akiishi naye walifuatilia suala hilo na kesi hiyo ikafutwa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
Nyota huyo anayeshughulia pia na utashaji wa muziki anasema hizo ni changamoto katika maisha yake ambayo hatamani kuyakumbuka na kuwela wazi kuwa aliachia wimbo wake wa kwanza 2009 uliokuwa ukiitwa 'Zaina' katika studio ya Buhemba iliyokuwa mkoani Mara.
Mkali huyo anayemzimia msanii Abbas Hamisi '20 percent' kwa sababu ya umahili wake katika utunzi na uimbaji anasema, baada ya kuachuia kibao hicho wafadhili walikisikia na kumsaidia kwenda studio kutengeneza nyimbo nyingine.
Anasema baada ya kwenda studio alifanikiwa kuachia kibao kingine kilichokwenda kwa jina la 'Nipe Nafasi' na Mamuwada katika studio ya KGT na kufanikiwa kutambulika vizuri kwa mashabiki wa muziki huo.Best Naso, alifanikiwa kuipua albamu yake ya kwanza mwaka jana 2010 iliyokuwa na nyimbo 14 zikiwemo Mamuwada ambayo ilibeba jina la albamu hiyo, Umedata
na pesa zao, Tuliza, Chekocheko na nyinginezo na anakili kuwa haikufanya vizuri katika soko la muziki.
Alisema baada ya albamu hiyo ya Mamuwada kutofanya vizuri kwa sababu mbalimbali alijiweka sawa na kuandaa albamu ya pili ambayo tayari iko sokoni.Anasema katika albamu hiyo ya pili yenye nyimbo 12, anaamini itafanya vizuri kutokana kutunga mashahiri yenye ubora na ujumbe mzito katika jamii.
Best Nasso akiwa katika pozi
No comments:
Post a Comment