Na Asmah Mokiwa
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi, ameitaka kamati aliyoiteua kuhakikisha wanasaidia kukamilisha mchakato wa kupata vazi la taifa.
Alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua kamati ya kukamilisha mchakato wa kupata vazi la taifa.
Dk Nchimbi alisema kamati hiyo inakazi kubwa kwani lazima ifikie mwisho wa kupata kitu ambacho Watanzania wamekua wakikisubiri kwa muda mrefu.
Alisema baada ya kupata vazi hilo, kamati hiyo itasaidia kulitangaza ili wananchi wajue ni kitu gani ambacho kinawatambulisha katika sekta ya mavazi.
"Wazo la kwamba ni vigumu kupata vazi la taifa linalokubalika na Watanzania wote ni la msingi sana, na ndio maana nikateua kamati hii, ambayo ndani yake kuna wataalamu wa nyanja tofauti, lakini muhimu katika kusaidia kukamilisha mchakato wa kupata vazi," alisema Dk Nchimbi.
Alisema wizara imeshafanya mambo kadhaa kuhakikisha inafanikisha zoezi hilo ikiwemo kutembelea nchi mbalimbali za kiafrika ili kupata uzoefu wa namna walivyopata mavazi yao ya Taifa.
Thursday, December 22, 2011
New
Dk Nchimbi awaamsha wanakamati vazi la taifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment