Na Asha Kigundula
KOCHA mpya wa timu ya Simba, Milovan Cirkovic amepatiwa kibali jana cha kufanya kazi nchini cha kuinoa klabu hiyo.
Kibali hicho kimetolewa na Idara ya Uhamiaji, kupitia katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambao walikikabidhi jana kwa uongozi wa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema jana kuwa klabu yao ina furaha kupata nafasi ya kufanya kazi na kocha huyo na kutoa wito kwa mashabiki na wanachama wao kumpa ushirikiano kocha wao Milovan.
"Leseni ya Milovan inaonesha kuwa ndiye kocha wa kiwango cha juu zaidi hapa nchini, hivyo sisi kama viongozi tunayo furaha kupatikana kwa kibali chake cha kufanya kazi nchini na tunaamini iataisaidia zaidi timu yetu," alisema rais huyo.
Wakati huo huo, Mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa Simba dhidi ya Eskom ya Malawi ambayo awali ilipangwa ifanyike Desemba 25, imeahirishwa, na sasa itafanyika Desemba 26.
Mabadiliko haya yametokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam ambazo zimeathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya watu, wakiwamo wapenzi wa kandanda na pia Uwanja wa Taifa wenyewe ambao mechi ilipangwa kuchezwa hapo.
"Simba, pia inapenda kutoa salamu za pole kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika na mvua hizo za Dar, Mara na Mbeya," aliongeza Rage.
Thursday, December 22, 2011
New
Milovan apata leseni kuinoa Simba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment