AWAMU SAID, Kinda wa Bom Bom anayetamani kukipiga Stars - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 22, 2011

AWAMU SAID, Kinda wa Bom Bom anayetamani kukipiga Stars

Hamisi Magendela
INAWEZEKANA kwa sasa linapotajwa jina la Awamu Said likawa geni kwenye masikio ya wanamichezo nchini kutokana na ugeni wake.
Japo sina shaka linapotajwa jina hilo mkoani Kagera kwenye wilaya Bukoba mjini kwa kila mwanamichezo unaekutana naye anaweza kukuelezea wasifu wa kinajana huyo mwenye miaka 19 kwa sasa.
Mwanandinga huyo anaeihusudu klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, Yanga, anasema alianza kucheza mpira wa miguu angali akiwa mdogo na kukukubalika vyema kwenye wilaya bukoba mjini.
Anasema wengi walioweza kumuona akicheza wakati huo walitabili kuwa anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji tegemezi katika soka la Tanzania kutokana na kuweza kuimudu vyema nafasi ya ushambuliaji.
Nyota huyo aliyehitimu elimu ya msingi mwaka 2007 katika shule ya Zamzam anasema, wakati akiwa katika kikosi cha timu ya Tumaini boys, Bukoba mjini alionekana na wadau mbalimbali wa soka na kufanikiwa kuchaguliwa katika timu ya mkoa chini ya miaka 17.
"Kujituma kwangu kulinifanya nichaguliwe kujiunga na kikosi cha timu ya Mkoa wa Kagera chini ya miaka 17 kutoka timu ya Tumani Boys hadi wilaya na baadaye timu ya Mkoa," anasema chipukizi huyo.
Chipukizi huo anasema baada ya kutakiwa kwenda Dar es Salaam na kikosi cha timu ya mkoa huo wazazi walikataa kutoa ruhusa hadi pale walipopelewa barua maalum kutoka Chama cha mpira mkoni humo.
Anasema kikosi hicho kilisafiri kwenda Dar es Salaam kushiriki mashindano ya vijana mwaka jana lakini hakikuweza kufanya vizuri kutokana na maandalizi kuwa hafiki.
Anatanabaisha kuwa katika mechi tatu alizocheza katika michuano hiyo walitolewa katika hatua ya makundi alifanikiwa kufunga mabao manne akiwa na wastani wa kufunga bao moja kwa kila mechi.
"Japo tulitolewa mapema lakini mashindano yale yalinipa uzoefu na ujasiri mkubwa wa kucheza mechi kubwa bila ya hofu na kufanya vizuri,"anasema Said
Kwa sasa kutokana na uhodari wake wa kufumania nyavu wadau mbalimbali wanaofika katika mazoezi ya timu yake ya sasa wanamfananisha na nahodha wa Arsenal, Robin Van Persie.
Anasema alipomaliza elimu ya msingi alichaguliwa kujiunga na shule ya sekondari Azania na wazazi wake kuhamia Dar es salaam na kujiunga na timu ya Bom Bom FC inayoshiriki ligi ya TFF Wilaya ya Ilala.
Mshambuliji huyo wa Bom bom Fc, anasema kujiunga na timu hiyo kumemfanya aanze kujulikana na kutokana na uhodari kuonesha kiwango cha juu katika nafasi ya ushambulia anayocheza.
"Nashukuru kwa sasa kuanza kuonekana tofauti nilivyokuwa nikicheza mpira mkoani kagera kwani kuonekana ilikuwa tabu kutokana na mashindano kuwa mchache tofauti na huku," alisema mchezaji huyo.
Anaweka wazi kuwa katika wachezaji wa kitanzania anavutiwa na Mrisho Ngaza wakati kutoka ulaya anamhusudu Chritian Ronaldo kutokana wanavyoweza kucheza na mipira na kumudu nafasi zao wanapokuwa uwanjani.
Mchezaji huyo anasema na kiu kubwa ya kucheza timu ya taifa na ili kufikia malengo hayo anafanya mazoezi ya kutosha na kumsikiliza kocha wake Kibonge katika timu yake ya sasa ya Bombom inayoshiriki michuano ya Ligi ya TFF Wilaya ya Ilala.
Pia anasema hadi kufikia hatua hiyo anawashukuru wadau mbalimbali waliomuwezesha kufikia kiwango cha kuweza kuoneka akiwemo kocha wake 'Kagila' wa timu yake ya zamani ya Tumaini Boys ya mkoani Kagera wilaya ya Bukoba Mjini.
0718594040.


Awadh Said kinda anaekipiga Bom Bom, timu inayoshiriki Ligi ya TFF Wilaya ya Ilala

No comments:

Post a Comment