Na Asmah Mokiwa
CHAMA cha Waamuzi Wilaya ya Kibaha (FRAT) kimewataka wadau wa mpira katika wilaya hiyo kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.
FRAT inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi kabla ya Januari 8, ambapo wanachama wa wilaya hiyo wanatakiwa kuchukua fomu za kuwania ili kukiletea chama hicho maendeleo ya mpira wa miguu.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Wilaya ya Kibaha, Pwani, Katibu Mkuu wa FRAT, Simon Mbelwa, alisema wanachama wa wilaya hiyo wanatakiwa kujitokeza ili kuwania nafasi hizo kwa maendeleo ya mpira wa miguu Mkoa wa Pwani.
Nafasi zinazowaniwa katika chama hicho ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe mmoja wa kuwawakilisha katika mkoa na kamati ya wajumbe watatu.
Alisema fomu za uchaguzi zinapatikana kwa waratibu wa wilaya ambapo katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu wake na Makatibu watalipia kwa sh 5,000, wakati wajumbe watalipa ada ya fomu hizo kwa sh 3,000.
Pia, Mbelwa aliwataka wanachama wa FRAT kulipa ada ya uanachama mapema kabla ya uchaguzi huo ili kupata haki yao ya msingi ya kuingia na kuchagua viongozi wao.
Friday, December 23, 2011
New
FRAT Kibaha waita wanachama wao
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment