ARAA wakaba koo katiba mpya - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, December 23, 2011

ARAA wakaba koo katiba mpya

Mahmoud Ahmad-Arusha
CHAMA cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), kimeingia katika kashfa nzito baada ya Mwenyekiti wake, Henry Nyiti kudaiwa kuchakachua katiba ya chama hicho, hali ambayo imezua mgogoro mzito.
Baadhi ya wajumbe na viongozi wa ARAA wamemtuhumu mwenyekiti wao, Nyiti kuwa ameshiriki kupitisha katiba batili kwa lengo la maslahi yake binafsi.
Wakizungumza na mwandishi wa blog hii hivi karibuni kwa nyakati tofauti bila kutaja majina yao hadharani, viongozi hao walidai Nyiti amepitisha katiba ambayo haina baraka kutoka kwao.
Walisema kuwa katiba iliyopo kwa sasa ni batili kwa kuwa haijapitishwa na mkutano mkuu wa chama hicho.
“Katiba ya sasa ni batili kabisa kwa kuwa sisi kama viongozi hatujaipa baraka na wala haikupitishwa na mkutano mkuu wowote na mwenyekiti wetu ana maslahi yake binafsi ndani yake,” walisema kwa nyakati tofauti.
Akijibu malalamiko hayo kwa njia ya simu jana, Nyiti alikanusha vikali na kudai kuwa hayo ni majungu yasiyo na tija, huku akisisitiza kuwa katiba iliyopo kwa sasa, awali ilikuwa na mapungufu madogo madogo, lakini amejitahidi kuyatatua.
Aliyataja baadhi ya mapungufu hayo ni pamoja na katiba hiyo kutogongwa muhuri na idara ya  usajili wa vyama vya michezo nchini, lakini tayari suala hilo liimeshatatuliwa.

No comments:

Post a Comment