MIKWAMBE ENGLISH MEDIUM PRE & PRIMARY SCHOOL WAANDIKA HISTORIA, WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, November 3, 2024

MIKWAMBE ENGLISH MEDIUM PRE & PRIMARY SCHOOL WAANDIKA HISTORIA, WAMPONGEZA RAIS DKT. SAMIA


Mgeni Rasmi katika mahafali hayo, Ofisa Elimu Kata ya Tuangoma, Kigamboni wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Jerome Mseye akikata keki, wa pili kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Eliza Mbeya na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule, Gervas Muyombe.


NA MWANDISHI WETU


SHULE ya Awali na Msingi Mikwambe, 'Mikwambe Medium Pre & Primary School' imefanikiwa kuandika historia kwa kufanya mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa Januari mwaka huu.


Katika mahafali hayo ambayo yamefanyika Novemba 2, 2024 katika viwanja vya shule hiyo iliyopo Mikwambe Kigamboni wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wazazi na walezi wametakiwa kulipa ada kwa wakati ili kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa uzio  kwa lengo kuweka mazingira ya ulinzi kwa wanafunzi.

.

Wito huo umetolewa na Ofisa Elimu, Kata ya Tuangoma, Jerome Mseye aliyemwakilisha Ofisa Elimu wa Temeke katika mahafali ya shule hiyo ya mchapuo wa kingereza inayomilikiwa na Serikali.




Katika mahafali hayo wahitimu wa darasa la awali 94 wamepatiwa vyeti tayari  kwa kujiunga darasa la kwanza mwakani,  wengine 30 wanarejea darasa la awali  kutokana umri wao kutowawezesha kwenda darasa la kwanza.



"Niwashukuru walimu wote kwa kazi kubwa ya kufundisha vema watoto hawa ambao leo wameandika historia kwa kuwa wanafunzi wa kwanza kuhitimu tangu shule hii kuanzishwa.


"Pia licha ya shule hii kuwa ya Serikali, kuna michango mingine inatolewa na wazazi kama ada ili kusaidia kuendeleza mambo mengi yaliyopo hapa ikiwemo ya kitaaluma hivyo niwaombe wazazi ada mlipe kwa wakati ili kusaidia utendaji kazi na kuleta ufanisi.


"Pia niwaombe wazazi na walezi kufuatilia nyendo za wao wakati wote wanapotoka nyumba, wanaporejea, wanapolala hadi kuamka lengo ni kuwajengea misingi bora katika maisha yao ni si kuwaachia walimu pekee," amesema.


Naye Mkuu wa shule hiyo, Eliza Mbeya, ameshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ambayo imepokelewa vizuri na wakazi wa wilaya hiyo.


"Nimshukuru Rais Dkt. Samia kwa  kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hii ambayo imevutia wazazi wengi kuleta watoto hapa, kutokana na uhitaji mkubwa kwa jamii tunamuomba tena Rais atujengee madarasa ya ghorofa ili tuwe na uwezo wa kuchukua wanafunzi wengi na kutumia nafasi ndogo katika ujenzi wa madarasa," amesema.


Amesema shule hiyo, imejengwa na Serikali na mafanikio yake ni makubwa kutokana na wazazi wengi kupeleka watoto wao hapo hali iliyofanya kuweka wastani wa alama A katika usahili wa wanafunzi.

Ameongeza kuwa wamesahili wanafunzi wa shule ya awali, darasa la kwanza, pili, tatu, tano na sita na wanaendelea kufanya vema na kuwa kivutio kikubwa kwa jamii kupeleka watoto wao hapo.

Pia amesema.shule hiyo, imepakana na shule kadhaa hivyo bila ya kuzungusha uzio wanapata changamoto kadhaa katika kuwalinda wanafunzi na kutoa wito kwa wadau kujitokeza kusaidia ujenzi wa ukuta.



Aidha amesema changamoto nyingine  kwao ni kwa baadhi ya wazazi kushindwa kulipa ada kwa wakati na kusababisha kushindwa kumalizia uzio wa shule hiyo na kulipa kwa wakati mishahara kwa walimu wa kujitolea ambao hawana ajira ya Serikali.i

Hivyo ametoa wito kwa wazazi ambao wenye changamoto ya kulipa ada kwa wakati kufika ofisini kwake kwa lengo la kujadiliana namna ya kufanikisha  ulipaji wa ada kwa wakati sahihi.


Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Gervas Muyombe kwa upande wake ameendelea kumshukuru, Rais Dkt Samia kwa kuwajengea shule hiyo.


"Zamani sisi kama wazazi tulikuwa tukijiuliza namna  tutakavyoweza kupeleka watoto wetu katika shule kama hii ya mchepuo wa kingereza kutokana na kuwepo kwa gharama kubwa.


"Hivyo Rais wetu, Dkt. Samia kutujengea  shule hii kwetu tunaona kama ni miujiza na ni maendeleo makubwa kwetu kupata shule hii,  tunawaomba wadau wa maendeleo kutujengea uzio ili kuweka mazingira mazuri ya kujisomea watoto, tuko tayari kupokea misaada mbalimbali ya vifaa vya kitaaluma na vya ujenzi wa uzio,"amesema.











No comments:

Post a Comment