KAMPUNI YA SUPER FEO NA SELOUS EXPRESS OMARY MSIGWA APEWA TUZO YA KUWAHUDUMIA WATANZANIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, September 3, 2023

KAMPUNI YA SUPER FEO NA SELOUS EXPRESS OMARY MSIGWA APEWA TUZO YA KUWAHUDUMIA WATANZANIA

                
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Super Feo na Selous Express Omary Msigwa.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya SITE TRUST FOUNDATION Juma Homera akimkabidhi Tuzo ya Omary Msigwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Wilman Ndile kwa ajiri ya kuikabidhi Kampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo ya Super Feo na Selous Express.


Tuzo ya Heshima iliyotolewa na Taasisi ya SITE TRUST FOUNDATION kwa Kampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo Super Feo na Selous Express kwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo

NA STEPHANO MANGO, SONGEA

MKURUGENZI wa Kampuni ya usafirishaji wa abiria na mizigo ya Super Feo na Selous Express, Omary Msigwa, amekabidhiwa Tuzo na Shirika la SITE TRUST FOUNDATION kwa kuwaletea watanzania maendeleo kusudiwa kupitia uwekezaji mbalimbali ambao ameufanya.

Juma Homera ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilolisilo la kiserikali la Site Trust Foundation amesema anatambua kazi kubwa ambayo inafanywa na Omary Msigwa katika kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inatekelezwa kwa vitendo.

Homera amesema kuwa, kwa kutambua hilo shirika lake limempatia Tuzo hiyo ya kuwa Kiongozi Bora, shupavu na jasiri kwa kuwahudumia wananchi katika sekta ya usafirishaji ,elimu, michezo na mazingira katika jamii kwa lengo la kukuza ustawi wa maisha yao ya kila siku kupitia vipindi mbalimbali ambavyo vinarushwa kwenye Redio yake ya Selous Fm 

"Omary Msigwa amekuwa ni kijana jasiri na shupavu katika kuanzisha na kuisimamia vyema kampuni yake na kutoa huduma ya usafiri kwenye maeneo ya mikoa mingi nchini na kuajiri watanzania wengi" amesma Homera.

Homera ameyasema hayo hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Songea wakati akiitambulisha taasisi hiyo kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambapo katika utambulisho huo uliohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Labani Thomas ,ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile

Amesema kuwa shirika hilo la Site Trust Foundation lina wajibu mkubwa wa  kumsaidia Rais Dkt Samia Suruhu Hassan kwa kugusa maisha ya wananchi wakiwemo wa Mkoa wa Ruvuma na kuwashika mikono wale wenye uhitaji ili kugusa maisha na kutimiza nia na ari ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwaletea ustawi  wananchi 

Wengine ambao wametunikiwa tuoz hiyo ni Dkt Damas Ndumbaro, Dkt Emmanuel Nchimbi Oddo Mwisho, Kanal Thomas Laban, na Rashid Tindwa.

Ameongeza kuwa wapo viongozi mbalimbali wastaafu na waliotangulia mbele za haki nao wametunikiwa tuzo ya kutambua mchango wao ambao waliutoa kwa nyakati tofauti akiwamo Dkt Laurence Gama, Rashid Mfaume Kawawa, Tani Tatu, Adam Kalumbeta

.Amefafanuwa kuwa katika sekta ya afya shirika hilo la Site Trust Foundation linajitahidi kuona umuhimu wa kuwafikia wananchi katika kuhamasisha na kuwaelewesha kufuata huduma ya afya kwenye vituo vya afya pia kusaidiana na Serikali kuhakikisha kuwa mazingira ya utoaji wa huduma yanaendelea kuboreshwa kama ilivyo adhima ya serikali ya awamu ya sita ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

”Ndugu mgeni rasmi mazingira ni uhai na shirika letu lisilo la kiserikali la Site Trust Foundation linaamini utunzaji wa mazingira ndio mtaji wa kizazi chetu kijacho ,hivyo pamoja na utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira hususan kwenye vyanzo vya maji shirika litahakikisha pamoja na mambo mengine linakwenda kuongeza upandaji miti katika maeneo yetu yenye uoto wa asili yaliyoharibiwa”amesema Homera.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amesema kuwa maendeleo licha ya kuwa Serikali imejikita zaidi kuyaboresha katika sekta mbalimbali pia sekta binafsi ina msaada mkubwa katika kusaidiana na Serikali kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za kijamii zinaboreshwa na si vinginevyo.

Hata hivyo amewataka wananchi mkoani humo kutoa ushirikiano kwa shirika hilo ambalo linaonesha kuwa na dira ya kusaidia huduma mbalimbali za jamii kuanzia ngazi za chini wakiwemo mama lishe, wajasiliamali, wakulima pamoja na wafanyabiashara kwani shirika hilo litaweza kusukuma maendeleo ya wananchi mbalimbali wa mkoa huo

No comments:

Post a Comment