NA
MWANDISHI WETU
MWENYEKITI Taifa wa
Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema ni aibu kuwepo kwa Kura
ya Mapema kwa upande wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba mwaka huu Tanzania Bara na Zanzibar.
“Ni aibu kubwa kuwepo
kwa kura ya mapema inayopigwa Oktoba 28 na Oktoba 29, 2025 wanachi wote wenye
sifa ya kupiga kura ndio tunakuwa na jukumu hilo, sasa basi tunachaofanya sasa
ni kuhakikisha katika uchaguzi huo tunapata wawakilishi wengi ili sheria hiyo
ikabailishwe kwenye Baraza la Wawakilishi.
“Chama Cha Mapinduzi
kilipata nafasi ya kupitisha sheria hiyo baada ya CUF kususia uchaguzi wa
marudio mwaka 2016 na athari yake ni
kubwa, mwaka huu hatususii uchaguzi tunaingia kingangali ili tuweze kupata
Wawakilishi wa kutosha ili sheria wakaipiginie ibarishwe,” amesema Prof
Lipumba.
Prof Lipumba amebainisha
hayo leo Agosti 8, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya kufanyika
Mkutano Mkuu Maalumu wa kupitisha wagombea wa Urais.upande wa Tanzania pna
Tanzania Zanzibar waliopendekezwa na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho
Agosti 6 mwaka huu.
Ameongeza kwamba wagombea
waliopendekezwa kwa upande wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Gombo
Sambandito Gombo na Nkunyuntila Siwale kwa upande wa Zanzibar waliopendekezwa
kugombea nafasi hiyo ni watatu ambao ni Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa, Mhandisi
Hamad Masoud Hamad na Dkt..Mohamed Habib Mikidadi.
Wagombea hao
watapigiwa kura na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum ili kupata mgombea mmoja
atakayepeperusha bendera ya CUF katika kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka
huu.
Wakati huo huo, Prof.
Lipumba amesema katika mkutano huo, watazindua Ilani yao kwa ajili ya kutangaza
sera za chama kwa wananchi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ili wananchi waweze kuendelea
kukiamini na kukipa ridhaa ya kushika dola.
"Baraza kuu la
Uongozi Taifa limepokea na kupitisha rasimu ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu upande wa
Muungano,pamoja na rasimu ya Uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar na Kupitisha
wagombea wa ubunge,vilevile wagombea wa uwakilishi"amesema Prof.
Lipumba.
Aidha amesema kuwa
Ilani ya CUF imebeba maono ya kujenga Tanzania Mpya kupitia Serikali ya
umoja wa kitaifa yenye misingi imara,ya usawa, mshikamano, uwajibikaji, demokrasia ya kweli
na maendeleo jumuishi kwa watu wote.
"Ilani ya CUF
imejikita katika misingi yakuweza kuleta haki sawa na furaha kwa Wananchi
wote,kujenga uchumi jumuishi unao ongeza ajira na kuondoa umasikini,kuimarisha
misingi ya demokrasia na utawala wa Sheria kwa kupata katiba mpya inayotokana
na maoni ya Wananchi,kuweka msingi wa maendeleo endelevu kwa kufanikisha utekelezaji
wa malengo ya maendeleo endelevu(Sustainable Development Goals) ifikapo mwaka
2030.
“Pia Ilani yetu inatekeleza
Sera ya CUF ya kipato cha msingi ni haki ya kila Mtanzania kwa kuanza kuwalipa
wazee wote wenye miaka kuanzia 60 nakuendelea kipato cha kujikimu na tunaamini uchaguzi
huu ukiwa huru nawa haki wagombea wetu watapata Ushindi mnene kwenye uchaguzi
huo,” amesema.
No comments:
Post a Comment