KICHWA TEMBA CHAPATIKANA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 13, 2026

KICHWA TEMBA CHAPATIKANA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI


NA MWANDISHI WETU


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukipata kichwa cha marehemu James Temba kikiwa kimefukiwa chini ya ardhi katika eneo la Kitunda Kibeberu wilayani Ilala  huku mganga wa kienyeji akitiwa nguvuni kwa madai ya kuhusika na tukio hilo.



Taarifa hiyo, imetolewa hivi punde na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam (SACP) Jumanne Muliro na kumtaja mganga huyo wa kienyeji kuwa ni Said  Ally 31 Mzigua, mkazi wa Kitunda Kibeberu.


"Baada ya kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikisha vya vyombo vingine vya ulinzi na usalama na kufanya uchunguzi wa kisayansi tulifanikiwa kumkamata mganga huyo wa kienyeji na akatupeleka alipokifukia  na sasa hatua nyingine za kisheria zinaendelea kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ili haki ipatikana," amesema.


 Siku chache zilizopita mwili wa Temba ulipatikana ukielea kwenye maji Mto Msimbazi na baadae kuzikwa mkoani Kilimamnjaro bila ya kuwa na kichwa.


Temba enzi za uhai wake alikuwa mwanafunzi WA mwaka wa Pili katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam.



iyekuwa  mwanafunzi cha Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM mwaka wa Pili ambaye mwili wake ulikutwa umeelea kwenye maji.

No comments:

Post a Comment