TEMBO CARD YA CRDB YAMPELEKA MAKONGORO NYERERE CANADA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 13, 2026

TEMBO CARD YA CRDB YAMPELEKA MAKONGORO NYERERE CANADA



MBUNGE wa Mikoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere amekuwa miongoni mwa wateja watatu ambao wameshinda nafasi ya kwenda Canada kushuhudia Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu.


Wateja wengine wawili walioshinda tiketi ya ndege kwenda Canada kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia nchini Canada kupitia droo ambayo imepewa jina la Fainali za Kombe la Dunia 2026 Ndio Mpango Na Tembo Card Visa ni mahususi kwa wateja wanaotumia kadi ya banki hiyo kufanya matumizi mbalimbali ni Abdulauf Muta na Arun Lodhia


Wakati wateja hao watatu wakishinda tiketi hizo za ndege katika droo ya pili iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam, Kwa upande walioshinda Tv Smart inchi 85 ni Ester Kabakama, Amina Awadhi na Lusekelo Mwamwala.


Na kwa upande wake Meneja Mwandamizi kitengo Cha Kasi Ndugu Karinaton Chahe amesema CRDB ipo kwa ajili ya kutimiza ndoto za watanzania na tayari washindi ambao wamepatikana katika droo hiyo wataungana wengine kukamilisha mchakato huo


Ndroo ya mwisho itafanyika mwezi ujao ambapo wateja wa benki hiyo wameombwa kuendelee kutumia Tembo Card katika kufanya manunuzi mbalimbali ili waweze kupata za ushindi.



Awali, wateja wawili kati ya watatu walioshinda Tv katika droo ya kwanza iliyochezeshwa mwezi uliopita ambao ni wakazi wa Dar es Salaam walikanishiwa zawadi zao ambao ni Samson Mkumbo, Theresia  Mawala.


Washindi hao sita ambao wamepatikana leo wanaungana na wengine saba waliopatikana April mwaka huu ambao watasubiri washindi wengine watakaopatika kwenye ndroo ya Juni mwaka huu ili kuendelea na mchakato WA safari na wengine kupewa zawadi ya TV smart inchi 85.

No comments:

Post a Comment