Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Msafara wa mwanamuziki wa bongo fleva, Ally Kiba amesimamisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa zaidi ya saa tatu mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini kuchukua tunzo yake ya Msanii bora barani Afrika.
Kiba ambaye aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa JNA majira ya saa nane mchana na kulakiwa na wapenzi lukuki ambao aliambatana nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Msafara huo ambao ulianzia katika barabara ya pugu kasha kuingia katika barabara ya Mandela na kuwapa fursa wakazi wa buguruni na viunga vyake vya malapa na bungoni kushuhudia msanii huyo akiwa katika gari ya wazi huku akionyesha tunzo yake huku wakazi hao wa jiji wakimshangilia.
Kiba alipita katika eneo alilozaliwa la Kariakoo mtaa wa Muheza na kumkabidhi mama yake tunzo hiyo na majirani zake ambao walipiga shangwe ya kutosha kutokana na mafanikio ya msanii huyo.
Msafara wa msani huyo ulitoka kariakoo na kupita katika mitaa ya Msimbazi, Upanga na barabra ya Sarenda kasha kuelekea moja kwa moja katika hotel ya Double Tree Masaki kwa ajili ya mahojiano na waandishi wa habari.
Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika
Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake.
Ally Kiba akiwa na ndugu yake Abdul Kiba juu ya gari la wazi katika mita ya Buguruni
Ally Kiba akimkabidhi Tunzo yake Mama yake mzazi maarufu kama Mama k
Mama K ambaye ni mama mzazi wa Ally Kiba akionyesha Tunzo ya msani huyo juu.
No comments:
Post a Comment