Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini
kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi
la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika
Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi
zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine
ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea
katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi
kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote
Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga,
jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo,
Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha
katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi
Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji
wataondolewa katika nyadhifa zao.
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya
kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya
Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi
hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga,
jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru
Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za
Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi
wa magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo
jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith
Mallya.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi
kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza na Wakuu wa Vituo vya Magereza yote
Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga,
jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo,
Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha
katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato
zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji
wataondolewa katika nyadhifa zao.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto
waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga (kulia
waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika
picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo,
kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu
wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi
hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Suleiman Msuya
NAIBU Waziri wa Mambo
ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni amesema Serikali haitasita kuchukua
hatua kwa wakuu wa magereza nchini ambao watashindwa kutimiza dhana ya
uzalishaji mali ambayo ni agizo la Rais John Magufuli.
Aidha, Jeshi la
Magereza Tanzania limetaja changamoto tano kuu ambazo zinakabili jeshi hilo
hali ambayo inakwamisha ufanisi katika mipango yao.
Masuani alisema hayo
wakati akizungumza katika mkutano wa wakuu wa vituo vya magereza Tanzania Bara unaofanyika
katika Bwalo la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri alisema
iwapo wakuu wa magereza watatumia wafungwa waliopo uzalishaji utaongezeka hivyo
kuondokana na tabia ya kulalamika ufinyu wa bajeti.
Alisema pamoja na vigezo
mbalimbali vya kupima wakuu wa magereza kigezo kingine kitakuwa ni kuangalia
kasi ya uzalishaji kwa eneo husika.
Masauni alisema jeshi
la magereza lina rasilimali mbalimbali kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa
kutumia fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.
“Napenda kuwa muwazi
hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza
fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo
vilivyopo katika wizara yetu,” alisema.
Naibu waziri alisema
anaamini kupitia jeshi hilo ajira zitaongezeka, uchumi utakuwa na maendeleo ya
nchi yatapatikana kwa haraka hivyo lengo la 2025 kukamilika.
Kwa upande wake
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk. Juma Malewa alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto
mbalimbali kama ufinyu wa bajeti, madeni ya watumishi, makazi duni, ukosefu wa
posho na vitendea kazi kama usafiri.
Alisema katika kutatua
changamoto ta usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni kati ya
905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.
Dk. Malewa alisema pia
wameanza kutatua changamoto ya makazi ambapo Rais Magufuli ametoa sh. bilioni
10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 320 katika kambi ya Ukonga.
Kamishna Jenerali
Malelwa alisema hadi sasa wamepokea sh. bilioni 5 ambazo zimeanza kutumika
kujenga nyumba hizo 320 zinazojengwa na
Wakala wa Majengo nchini (TBA).
Alisema wao wamejipanga
kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inapatikana kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali hivyo utatuzi wa changamoto hizo utakuwa suluhu sahihi kwao.
“Tumedhamiria kuongeza
uzalishaji na kufufua viwanda mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
lakini tunaomba changamoto nilizozitaja zitatuliwe kwa wakati,” alisema.
Akizungumzia dhana hiyo
ya viwanda Mkurugenzi wa Viwanda, Naibu Kamishna wa Magereza Edith Mallya
alisema utekelezaji wa agizo la Serikali umeanza katika baadhi ya viwanda kama
Mbigiri Morogoro na Karanga Moshi.
No comments:
Post a Comment