MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA KAZAMOYO APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 14, 2017

MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA KAZAMOYO APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA


ISOO
KAMANDA wa polisi mkoani Pwani, Boniventure  Mushongi,anaehamia mkoa wa Simiyu akizungumzia tukio la  mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo huko Rufiji (Picha na Mwamvua Mwinyi).


Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAUAJI kwa viongozi wa vijiji na vitongoji mkoani Pwani hususan wilayani Rufiji vimeendelea kukua ambapo mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo wilayani humo Hemed Njiwa (45) ameuawa kwa kupigwa risasi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi ambae anahamishiwa mkoa wa Simiyu alisema marehemu aliuawa na watu wasiojulikana  wakati akiwa nyumbani.
Tukio hilo lilitokea  usiku wa kuamkia machi 13 ,eneo la Kifuru kata na tarafa ya Ikwiriri wilayani hapo.
“Marehemu alipigwa risasi kifuani akiwa nyumbani kwa mke wake mdogo Maimuna Abdallah (36) na alikutwa na jereha la risasi kwenye mkono wake wa kushoto”
Kamanda Mushongi, alieleza kwamba mtu ama watu aliyehusika na tukio hilo baada ya kumwua alikimbia kusikojulikana kwa kutumia pikipiki aina ya boxer ambayo haikuwa na namba za usajili.
Alisema hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na jeshi la polisi linaendelea na msako mkali ili kuweza kubaini watu waliohusika na tukio hilo.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuwafichua watu wanaohusika na matukio ya kuua viongozi wa vijiji na vitongoji kwani hilo linaweka idadi ya matukio zaidi ya matatu yaliyohusisha viongozi hao.

No comments:

Post a Comment