WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA MFUKO WA LAPF - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, March 12, 2017

WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA MFUKO WA LAPF


1Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama akizungumza katika mkutano mkuu wa 9 wa wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Watumishi wa Serikali za Mita,(LAPF) jijini Arusha.

2

Mkurugenzi wa KeyMedia Agency ya jijini Arusha   akiwa katikati Bi.Barbra Keiya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa LAPF, kampuni hiyo ilibeba  jukumu la kualika vyombo vya habari kwaajili ya mkutano huo



Na Pamela Mollel, Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama amewataka vijana kujiepusha na madawa ya kulevya ili utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda ilete ajira kwa vijana wenye nguvu

Aliyasema hayo jijini Arusha wakati akifunga mkutano mkuu wa9 wa wadau
 wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa serikali za mita,
 LAPF uliohudhuriwa na wadau wa mfuko huo

Alisema kuwa kwa sasa serikali imedhamiria kuwainua idadi kubwa ya vijana waliona ujuzu mdogo kwa kuwajenge uwezo kupitia mafunzo mbalimbali katika vyuo vilivyopo nchini

”Udhibiti mkubwa wa madawa ya kulevya unahitajika kwa vijana wetu ili kutengeneza taifa lenye nguvu ya kufanya kazi ”alisema

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana ujuzi wa kutosha hivyo basi serikali ya awamu ya 5 imejipanga ipasavyo kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia viwanda

Hata hivyo aliipongeza mfuko wa LAPF kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiitaka mifuko yote ya kijamii hapa nchini ihakikishe kuwa ifikapo 2025 inakuwa na wanachama wengi zaidi

No comments:

Post a Comment