NA MAGENDELA HAMISI
NAIBU Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesisitiza kwa uongozi wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuhakikisha mitaala yao katika kozi zinazotolewa chuoni hapo zitoe mbinu sahihi ya kudhitibiti wizi wa mitandaoni.
Pia ameweka wazi kuwa ni dhahiri mchakato unaoendelea wa kutoa elimu kwa kutumia mfumo kidigitali, wanafunzi wanapohitimu masomo yao kwa ngazi mbalimbali na wakiwa na mbinu imara wa kudhitibiti wizi wa mitandaoni itasaidia kuhimalisha uwekezaji ulipo na kuwa endelevu.
"Changamoto kubwa ambayo inayotukabili kwa sasa ni kufanya uwekezaji uliopo kuwa endelevu, hivyo msaada mkubwa wa kuhakikisha hilo linafanikiwa na Chuo kutoa wataalamu ambao wameiva kutika mifumo ya teknolojia ya kigitali," amesema.
Naibu Waziri Kigahe, alisisitiza hilo leo, jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 18 kwenye mkutano wa kidigitali wa kuadhimisha miaka 50 ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake na kutoa wito kwa wadau wa sekta ya fedha na bima, kujikita kwenye teknolojia ya kidigitali ili kuwa na uwekezaji wenye endelevu.
Katika Mkutano huyo, Naibu Waziri Kigahe, alimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, pia mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa na wadau wa taasisi za fedha, bima, vyuo vya fedha ikiwamo wawakilishi kutoka serikalini.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof, Joseph Lotta, alibainisha kuwa wameanzisha kozi ambazo zimo kwenye mfumo wa kidigitali kwa lengo la kuhakikisha uhalifu mtandaoni unadhibitiwa hususan katika sekta za bima na fedha.
Pia alibainisha kuwa wapo katika mchakato wa kuhakikisha mwaka ujao wanaboresha mitaala ya masomo katika ngazo zote za elimu kwa la lengo la kuwapa ujuzi wataalamu ndani ya sekta hizo, kukabiliana na wizi wa mtandaoni katika sekta ya fedha.
"tunachofanya sasa ni kuendana na mahitaji ya mabadiliko ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye sekta ya fedha hususan kwenye mifumo ya kidigital na ni dhahiri tunakwenda kufanikiwa na kuwa mfano kwa mataifa mengine na itasaidia kuvutia wawekezaji wengi nchini , alisema.
Pia alitoa wito kwa wanafunzi na wahitimu kutumia mitandao vema kwa manufaa ya taifa na si kuitumia vibaya jambo ambalo litakuwa kinyume na matarajio wanayohitaji.




No comments:
Post a Comment