BRELA YATOA ELIMU YA MILIKI BUNIFU KWA WAFANYABISHARA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, January 19, 2023

BRELA YATOA ELIMU YA MILIKI BUNIFU KWA WAFANYABISHARA

                                                                                                  



 Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu kutoka BRELA , Seka Kasera, akizungumza na waandishi wa Habari.

NA MAGENDELA HAMISI

WAFANYABIASHARA nchini wametakiwa kulinda na kutumia vema alama zao za biashara na Huduma ili kulinda uchumi na kuondoa migogoro ya kubaina yao wafanyabishara wengine wakiwamo wanaokuja nchini kununua bidhaa na kuzipeleka nje.
Wito huo umetolewa leo na Seka Kasera, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakati akifungua kongamano la Jumuia la wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.
Katika kongamano hilo alisisitiza kuwa wafanyabishara wanatakiwa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu alama za biashara ili kuhakikisha wanapata mafanikio kupitia shughuli zao na kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla.
"Leo tumekutana na viongozi wa Jumuiya za wafanyabishara kupitia jumuia zao wakiwamo wanachama wa STI, TPSF,TCCIA na Jumuiya ya Wafabishara Kariakoo ikiwa ni sehemu ya mkakati wetu kuhakikisha tunakutana na kubadilisha mawazo ili kuweka mikakati ya pamoja ili kufikia malengo," amesema.
Aliongeza kuwa ili nchi isonge mbele inahitajika teknolojia ya hali ya juu ya Miliki Bunifu na kwa kuwa  Tanzania ya sasa ni ya viwanda, hivyo wamiliki wa viwanda na wafanwanatakiwa kuuza bidhaa zao kwa kutumia alama zao za biashara.
Alibainisha kuwa wafanyabishara wengi wanatoa bidhaa nje ya nchi hivyo wanatakiwa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu Miliki Bunifu na kuzilinda ili kusaidia kupunguza migogoro ya kugombania alama za biashara.
Aliongeza wafanyabiashara watakapofanikiwa kulinda alama zao za biashara watasadia kulinda viwanda vya ndani kwa kutoingizwa kwa bidhaa feki ambazo zimekuwa zikiyumbisha uchumi wa nchi.
Pia alibainisha kuwa baada ya kutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara wa Dar es Salaam kupitia vyama vyao, watakwenda mikoani na wataanza na mikoa ya Kanda ya Ziwa na Mbeya ambapo watakutana na jumuia za wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Kasera alibainisha kuwa elimu hiyo itasambazwa nchini kote kupitia wafanyabiasha wadogo na wakubwa ili kutimiza malengo ambayo yamekusudiwa ikiwamo kuongeza thamani ya bidhaa na kuzilinda.
"Lengo ni kuhakikisha wanafanyabishara wanafanya vema katika nyanja za biashara ndani na nje ya nchi ili kuinua uchumi wetu na wanaponunua bidhaa za nje waweze kudhibiti vema wanapoziuza kwa wengine," amesema.
Kasera aliweka wazi kuwa mbali na kuendelea kufanya mchakato huo wa kutoa elimu kwa wafanyabiashara pia wanajipanga kushindanisha wanafunzi kuanzia ngazi ya Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu ili kupata wanafunzi wabunifu ambao watasaidiwa kutafutiwa masoko na kuendelezwa.
Kwa upande, Martine Mbwana, ambaye ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, ambaye ameshiriki mafunzo hayo amesema kuwa Brela kutoa mafunzo hayo kwa jambo jema ili akawataka kufika katika maeneo yao ya biashara ili kuzungumza na wafanyabishara.
"Nashukuru kwa Brela kutukumbuka lakini ni vema wakafika katika maeneo yetu ya biashara ili kutoa elimu hii kwa pamoja ili kila mfanyabiashara imfike moja kwa moja kupitia maafisa wa Brela," amesema.

No comments:

Post a Comment