NA MAGENDELA HAMISI
KAMPUNI ya Sanlam General na Sanlam Life Insurance Tanzania, imemzawadia gari wakala wa wake, Gilda's Rwiza, baada ya kuibuka mshindi kwa mwaka 2022 wa kupitia shindano la Vuna Pointi.
Katika harakati za kuthamini juhudi zinazowekwa na mawakala wao, kampuni hiyo imekuwa ikitoa zawadi ikiwamo fedha taslimu, pikipiki, kupitia programs inayofahamika kwa jina la Vuna Point.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo Cha Biashara na Masoko, Charles Magori, mchakato huo ni mahusus ili kutambua na kutunuku juhudi zinazofanywa na mawakala katika kuhudumia wateja Sanlam.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Anjelina ambaye amejishindia pikipiki mpya kutoa hamasa kwa kutoa hamasa kwa mawakala wengine kujituma zaidi na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya ushindi kwa mwaka huu.
Naye, Rwiza, alisema kuwa anashukuru kuwa mshindi wa kwanza katika shindano na ushindi huo umempa nguvu ya kujituma na kufanya vema kwa mara nyingine.




No comments:
Post a Comment