WAKULIMA ZINGATIENI MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA - TFRA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, July 8, 2023

WAKULIMA ZINGATIENI MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA - TFRA

   

Mkurugenzi Mtendaji  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo  (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo alipotembelea banda    hilo kujionea shughuli za   maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara  (Sabasaba)  yanayoendelea jijini Dar es Salaam.







MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), imetoa wito kwa wakulima nchini kuzingatia utaratibu wa matumizi sahihi ya mbolea ili kuleta tija katika kilimo.

Kaimu Meneja wa TFRA Kanda ya Mashariki, Allan Mariki, alisisitiza hilo katika viwanja vya Maonesho ya 47 Sabasaba  jijini Dar es Salaam, pia ameongeza kuwa kabla ya kuanza kilimo ni vema wakapima udongo husika ili kufahamu ni zao gani ni sahihi kwa udongo huo.

“Kwa ujumla mmea unapofikia siku 21 unahitaji virutubisho vya nitojen kwa wingi kulingana na mbolea iliyowekwa ya kupandia ingawa tunashauri zaidi itumike mbolea ya ESE ambayo inavirutubisho kwa kwa wingi vya nitojeni,” amesema .

Ameongeza kuwa mmea ili ukue vizuri unahitaka mbolea tofauti za aina tatu ambazo ni ya kupandia, kukuzia na kuzalishia jambo ambalo ametoa wito kwa wakulima kutumia zaidi mbolea ya NBK ambao inavutubisho vyote kwa wakati mmoja.

Pia amesema kuwa mkulima anaweza kutumia mbolea yoyote ile kwa usahihi kabisa lakini siku ya mwisho asipate matokeo yanayohitajika kutokana na kutojua kiwango sahihi cha PH cha udongo, hivyo akataka kupima udongo kabla ya kuanza kilimo.

Amesema kwamba kufahamu changamoto za udongo kabla ya kuanza kilimo inasaidia kujua aina ya mazao yanayohitajika katika eneo husika kutokana na kiwango cha PH kinachohitajika katika udongo huo.

Malik, ameongeza kwamba mazao mengi yanahitaji kiwango cha PH 5.5 hadi 7katika udongo ingawa yapo baadhi ya mazao yanahitaji chini ya kiwango hicho au cha juu, hivyo ni vema udongo kupimwa ili kupata matokeo chanya katika kilimo.

Amesisitiza kwamba pindi changamoto zinapoonekana, mkulima anaweza kutumia mbolea ya visaidizi vya udongo inayosaidia kurekebisha tindikali iliyomo kwenye ardhi kabla ya kuanza kilimo.

 Pia amesema licha ya mkulima kutakiwa kufuata mazingatio ya matumizi sahihi ya mbolea katika hatua ya ukuaji wa mmea pia anatakiwa kuhakikisha anaandaa shamba na kulifuatilia kwa ubora unaotakiwa.

“Mfano uwezi kuweka mbolea wakati mmea haujapaliliwa maana yake majani au magugu yatakua sehemu ya matumizi ya mbolea jambo ambalo ni kinyume na malengo husika,” amesema.

Ukiachana na hilo, pia amesema kwamba mkulima anatakiwa kuweka mbolea kwenye mmea kipndi cha unyevunyevu na si kipindi cha mvua kwa maana mbolea inaweza kuondoka kwa mafuriko na jambo lingine ambalo linatakiwa kuzingatiwa na mbolea kuwekwa wakati jua likiwa limepoa si wakati wa jua kali.

“Mbolea ikiwekwa wakati wa jua kali itasababisha mmea kuungua hivyo ni vizuri mkulima akazingatia mambo hayo kabla na wakati wa mwendelezo kabla ya kuvuna mazao,” amesema.

Naye Esther, Kapakala ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa Udhibiti wa Ubora wa mbolea kutoka TFRA, amesema kuwa moja ya jukumu lao ni kuhakikisha wanahamasisha wawekezaji kuwekeza katika viwanda vya mbolea nchini ili kupunguza gharama za uingizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi.

“Wakati inaanzishwa TFRA, kulikuwa na kiwanda kimoja tu nchini na kwa sasa kuna viwanda vikubwa na vidogo vya mbolea 17 ambavyo vinazalisha mbolea ya kuchanganya jambo ambalo tunaweza kusema tumeanza kupiga hatua kwenye uwekezaji wa viwanda nchini ingawa bado juhudi kubwa ya uhamasishaji inahitajika ili wadau waje kujenga viwanda hapa nchini,” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na juhudi kubwa ya uhamasishaji zinayofanywa na Mamlaka, wamefanikiwa kupata mwekezaji mkubwa ambaye amewekeza katika kiwanda cha mbolea kilichopo jijini Dodoma, lengo likiwa ni kuzalisha mbolea kwa wingi nchini.

Pia amesema kuwa hadi sasa Tanzania inaagiza mbolea kutoka nje ya nchi kwa asilimia 90, hivyo inatoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza katika sekta ya viwanda vya mbolea nchini.


No comments:

Post a Comment